Moja ya biashara ambayo imeshamiri katikati ya miji hasa Dar es salaam ni biashara ya mihogo mibichi, nazi na karanga mbichi. Kwa utafiti mdogo kwa njia ya kuuliza watumiaji na wauzaji wanasema kuwa vyakula hivyo vinaongeza mbegu za kiume.
Leo nitawaletea maelezo ya kitaalamu ni aina gani ya vyakula ambavyo husaidia kuongeza idadi ya mbegu za kiume zenye afya na ujazo wake na faida zingine za afya ya uzazi.
Mayai ni moja ya vyakula vinavyokubalika kitaalamu kusaidia kuongeza wingi wa mbegu za kiume na vile vile kusaidia kuongeza kasi ya mbegu za kiume kutokana na mayai kusheni vitamin E na protini, ambayo vyote kwa pamoja husaidia kulinda mwili kutokana na sumu za radiko ambazo hupunguza wingi wa mbegu za kiume.
Vilevile virutubisho hivyo vilivyopo katika yai husaidia kutengenezwa kwa mbegu imara zenye afya jambo ambalo ni muhimu kwa urutubishaji wa kijiyai cha kike.
Spinachi ni moja ya mbogamboga ambayo inakubalika kusheheni tindikali ya foliki ambayo ni muhimu sana katika utengenezwaji wa mbegu za kiume, ingawa mboga zote za kijani zinakubalika kutokana na kusheheni vitamini mbalimbali.
Pale mwanaume anapokuwa na kiwango kidogo cha foliki, husababisha kuzalisha mbegu za kiume zisizo timilifu. Mbegu za namna hii zinakuwa na wakati mgumu katika kufikia na kupenya katika tando za kijiyai cha kike wakati wa urutubishaji. Hali kama hii inaweza kusababisha kuzaliwa mtoto mwenye hitilafu za kimaumbile kwa sababu ya kijiyai cha kike kurutubishwa na mbegu zenye hitilafu.
Ndizi ni moja ya tunda ambalo limesheheni vitamin A, B1, na C ambazo husaidia mwili kutengeneza mbegu za kiume zenye afya na vile vile kuongeza wingi wa mbegu hizo. Pia, ndizi huwa na kimeng’enya adimu kijulikanacho kitabibu kama Bromelain ambacho huzuia milipuko wa kinga ya mwili, hivyo husaidia kuongezeka wingi wa mbegu za kiume pamoja na kasi yake.
Chokoleti yenye rangi ya kahawia iliyokolea inajulikana zaidi duniani na ndiyo maana katika hoteli kubwa huweka ndani ya vyumba vya wanandoa waliopo fungate. Sababu kubwa ni kutokana na aina hii ya chokoleti kuwa na tindikali ya amino (protini) ijulikanayo kama L-Arginine HCL ambayo husaidia kuongeza ujazo wa mbegu za kiume na wingi wake. Vilevile huongeza msisimko wa kilele cha tendo la ndoa.
Mboga ijulikanayo kama Asparagus ambayo huwa na kiasi kikubwa cha Vitamin C ambayo ina wigo mkubwa katika kusaidia utengenezwaji wa mbegu za kiume. Vitamin C hutoa ulinzi kwa seli zilizopo katika kokwa za kiume (kende) zisidhuliwe na radiko huru, hivyo kufanya kiwanda cha mbegu za kiume kutengeneza mbegu zenye afya na zenye uwezo wa kupiga mbizi kwa kasi.
Broccoli ni aina ya mboga ambazo zipo hapa nchini ingawa si maarufu kwa Watanzania, ila katika migahawa ya Magharibi na ya Kichina, mboga hii yenye kufanana na uyoga inasifika kutokana na kuwa na kiasi kikubwa cha foliki ambayo hujulikana pia kama vitamin B9. Vitamin B9 ilishajulikana kwa kusaidia wanawake waliokuwa wagumba kuweza kushika ujauzito, kwa sasa pia inajulikana kusaidia wanaume wagumba.
Tunda la komamanga ambalo lipo pia katika jamii yetu linajulikana kusaidia kutengenezwa idadi kubwa ya mbegu za kiume zenye ubora.
Post a Comment
Post a Comment