Msimu ulioisha wa ligi pamoja na kuwekeza pesa nyingi sana katika usajili na kununua baadhi ya wachezaji wakubwa lakini klabu ya Ufaransa ya PSG ilishuhudia ikipoteza kombe la Ligue 1 ambapo kombe hilo lilienda kwa timu ya Monaco.
Patrick Kluivert alikuwa mkurugenzi wa masuala ya ufundi katika timu hiyo na ameamua kubwaga manyanga, Kluivert ambaye ameshawahi kuvichezea vilabu vya Ajax,Ac Millan na Barcelona amedumu katika ukurugenzi huo kwa muda mfupi wa msimu mmoja tu.
Haijawekwa wazi sana sababu za Kluivert kubwaga manyanga lakini inaonekana wazi wazi kwamba kitendo cha Monaco kuumaliza ubabe wa PSG na matokeo yao katika Champions League ndio sababu kubwa kwa Kluivert kuachia ngazi kwani hata mabosi wa timu hiyo hawakufurahishwa na mwenendo wa timu hiyo tangu Kluivert apewe jukumu hilo.
Raisi wa klabu ya PSG Nasser Al Khelaifi amesema kocha wa klabu hiyo Emery atabaki kuwa kocha wao lakini akimshukuru Kluivert kwa kazi aliyoifanya akiwa klabuni hapo”tunamshukuru Patrick kwa kazi kubwa aliyofanya akiwa na sisi na tunamtakia kila la kheri kwa kile alichoamua kukifanya katika miaka ijayo” alisema Khelaifi.
Msimu huu PSG wameshinda Coupe de France na Coupe de la Ligue pekee matokeo ambayo hayakuwa mazuri na yalimfanya Kluivert na kocha Unai Emery kuonekana kama wanaiangusha timu na hivyo Patrick Kluivert kuamua kuachana na timu hiyo.
Post a Comment
Post a Comment