Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Naibu Waziri Wa Mambo ya Ndani Massauni amefunguka na kusema hivi sasa madereva ambao watakuwa wakikiuka makosa ya barabarani wanapaswa kuchukuliwa hatua kali ikiwezekana hata kuchalazwa viboko.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Hamadi Massauni
Massauni amesema hayo leo wakati akitoa taarifa ya tathimini ya utekelezaji wa mpango wa mkakati wa kupunguza ajali barabarani nchini kwa asilimia 10 katika kipindi cha miezi sita kuanzia Agosti 2016 hadi Januari 2017.
"Suala la kwanza tunataka kulipa kipaumbele ambalo hatukufanikiwa katika mkakati wetu wa kwanza ni kuhusu NUKTA katika leseni za udereva tulisema tuanze lakini hatukufanikiwa lakini suala la pili ni kuchukua hatua kali dhidi ya madereva wanaokiuka sheria za usalama barabarani, ikibidi hata kuwachapa viboko maana lazima muda mwingine twende hivyo hatua zitakuwa kali sana safari hii" alisema Massauni
Mbali na hilo Massauni alisema pia watu wengine ambao wanapaswa kuchukulia hatua kali ni pamoja na wauzaji wa pikipiki ambao wanauza pikipiki bila kubadilisha usajili na umiliki wa pikipiki zao na kuziuza, pia na watu ambao wanamiliki leseni za udereva ambazo ni feki wanatakiwa kutafutwa na kukamatwa.
Post a Comment
Post a Comment