Meya wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro, amempa siku saba Mkuu wa Mkoa Arusha, Mrisho Gambo kumwomba radhi yeye na viongozi wa dini aliowaweka ndani wakati wakijiandaa kupokea rambirambi ya wafiwa wa wanafunzi wa shule ya Lucky Vincent.
Akizungumza leo na waandishi wa habari Arusha, Meya Calist amesema kitendo cha kuwakamata wakiwa wamekusanyika shuleni hapo Mei 18, mwaka huu, kilikuwa ni ukiukwaji wa sheria na kwamba kabla ya kuwakamata alitakiwa awe na amri ya mahakama inayofafanua ukamataji wao, lakini haikuwa hivyo jambo ambalo anadai kuwa ni matumizi mabaya ya madaraka
Hata hivyo Mh. Calist amesema kuwa Mh. Gambo asipofanya hivyo baada ya siku hizo atampeleka mahakamani kwa kuwadhalilisha na kuwaweka ndani bila kosa lolote kwa kuwa hadi sasa hawajaambiwa kosa lao lilikuwa lipi.
Post a Comment
Post a Comment