Mabingwa wa ligi kuu Italia klabu ya Juventus wameingia rasmi katika vita ya kumsaka mshambuliaji wa Leicester City Riyad Mahrez, mshambuliaji huyo wa Kialgeria anakaribia kuondoka Leicester huku Arsenal na Liverpool nao wakimtaka.
Wakala wa mshambuliaji Alvaro Morata aitwaye Juanma Lopez amezidi kuiaminisha dunia kuhusu tetesi za mteja wake kwenda Manchester United baada ya kuthibitisha kwamba mteja wake hawezi kwenda Ac Milan.
Klabu za Real Madrid na Manchester United itawabidi watafute golikipa mwingine baada ya Gianluigi Donnaruma ambaye walikuwa wakimtaka kuamua kubaki katika klabu yake ya Ac Milan huku akisisitiza hana mpango wa kuondoka.
Klabu ya Manchester City itakabiliwa na ugumu mkubwa kumnunua Alexis Sanchez kwani klabu ya Arsenal inaona ni hatari kumuuza Sanchez katika vilabu vya Epl na ni bora wamuuze Ujerumani katika klabu ya Bayern Munich.
Baada ya kuamua kuondoka katika klabu ya Chelsea sasa tetesi zinasema mlinzi wa zamani wa klabu hiyo John Terry anaweza kujiunga na klabu ya Aston Villa huku pia klabu hiyo ya Chelsea ikituma ofa ya euro 60m ili kuweza kumnunua mlinzi wa kushoto wa Juventus Alex Sandro.
Post a Comment
Post a Comment