Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Brazil na klabu ya Barcelona Neymar anaweza kuwa hayuko katika kiwango sawa na Lioneil Messi au Cristiano Ronaldo lakini nyota huyo wa Kibrazil ameendelea kukaa kileleni kwa wachezaji wenye thamani zaidi duniani.
Utafiti mpya uliuofanywa na shirika la CIES Football Obersavation unaonesha kwamba mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25 ana thamani ya euro 185m takwimu ambazo huangaliwa kutokana na umri wa mchezaji,kiwango chake,mkataba alionao,mvuto kwa vilabu na nafasi yake kimauzo.
Lakini katika orodha hiyo kungo wa klabu ya Tottenham Delle Ali yupo katika nafasi ya pili ambapo thamani ya Delle ni euro 136m, thamani ya Delle imeongezeka sana kutokana na kiwango anachokionesha haswa msimu uliopita akiwa na Tottenham Hotspur.
Chini ya Delle Ali yupo mchezaji mwingine wa Tottenham Hotspur ambaye pia ni mfungaji bora wa ligi kuu Uingereza Harry Kane ambaye thamani yake ni euro 135m huku Lioneil Messi akiwa nafasi ya nne na thamani ya euro 134m.
Nyota wa Atletico Madrid Antoine Griezman yuko nafasi ya tano akiwa na thamani ya euro 132m akifuatiwa na mshambuliaji wa klabu ya Barcelona Kuis Suarez ambaye ana thamani ya euro 124m.
Katika nafasi ya saba yupo kiungo wa klabu ya Manchester United anayeshikilia rekodi ya usajili ya dunia ambaye thamani yake ni euro 118m akifuatiwa na Gonzalo Higuain nafasi ya nane akiwa na thamani ya euro 106m.
Mshambuliaji hatari na mchezaji bora wa klabu ya Chelsea Eden Hazard mwenye thamani ya euro 104m akishika nafasi ya tisa na Paulo Dyabala anamaliza katika nafasi ya kumi ambapo thamani ya Dyabala ni euro 102m.
Gumzo kubwa limekuwa kwa Cristiano Ronaldo ambaye hayupo katika orodha ya 10 bora na jina lake linatokea nafasi ya 11 akiwa na thamani ya euro 99m huku mshambuliaji anayetaka kujiunga na Chelsea Romelu Lukaku akiwa na thamani ya euro 93m.
Post a Comment
Post a Comment