KENYA: Majambazi wamevamia nyumba ya Mchungaji eneo la Mweiga katika Kaunti ya Nyeri wakachinja kuku wake, wakampika na kumla na kisha wakaosha na vyombo walivyotumia.
Mchungaji Joseph Muraya alisema kuwa wezi hao waliingia katika eneo lake majira ya saa mbili usiku na kuwatisha kuwaua kwa kuwapiga risasi endapo wangewataarifa majirani zao.
Nilirudi nyumbani saa majira ya saa mbili na nilishangaa kukuta geti langu limefunguliwa nusu, nilisikia mbwa wana bweka na nilipokwenda kuwaangalia nilikuta mtu mmoja yupo nje, na baadae niligundua kuwa kuna wengine watano wamo ndani, alisema mchungaji huyo.
Majambazi hao baada ya kupika na kuosha vyombo, waliondoka na mali za ambazo thamani yake haijulikani.
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Nyeri, Peter Okiring alisema kuwa Jeshi la Polisi tayari limeanza uchunguzi kuwabaini wahalifu hao.
Post a Comment
Post a Comment