Mkuu wa wilaya ya njombe ruth msafiri ameziagiza halmashari za wilaya hiyo kuhakikisha zinasimamia unywaji wa maziwa kwa watoto shuleni kufuatia hali ya utamiamlo ambayo imekuqwa ikiwakumba watoto mara nyingi mkoani njombe kutokana na kukosa lishe bora.
Magizo hayo ameyatoa katika kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri ya mji njombe baada ya kupokea taarifa ya uzalishaji wa maziowa katika kiwanda kimoja mjini njombe ambacho kinamilikiwa na taasisi binafsi pamoja na serikali mkoani njombe.
Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa njombe anawasiwasi na hali ya afya kwa watoto wanaoishi mjini kwa kuwa mara nyingi wazazi wamekuwa wakishindwa kuchanguia hata mlo mmoja wa chakula cha mchana kwa watoto na kusalia wakilishwa makande.
uongozi wa kiwanda cha maziwa cefa cha mjini njombe umeamua kuwatumia madiwani ili wahamasishe wazai kukubali kutoa huduma ya maziwa mashuleni kufuatia mwamko mdogo uliopo
Na prosper mfugale njombe
Post a Comment
Post a Comment