WANANCHI NJOMBE WALALAMIKIA MRADI WA MAJI KUCHELEWA KUKAMILIKA
Wananchi wa kijiji cha Ngalanga Kata ya KIFANYA na Kijiji cha utengule Kata ya iwungilo Wilaya ya NJOMBE Mkoani NJOMBE waitaka serikali kukamilisha mradi wa maji ambao mkandarasi ameuterekeza tangu mwaka 2010 ulipoanza kutekelezwa na mkandarasi unaogharimu zaidi ya bilioni moja kwa ufadhili wa bank ya dunia.
Wakizungumza kwa masikitiko makubwa na itv katika vijiji hivyo wamesema serikali kupitia ngazi ya mkoa imekuwa ikitoa ahadi za maramara kuwa mradi huo ungekamilika mara moja na wanaishia kushuhudia mabomba na matenki yaliyojengwa ambayo yameanza kuchakaa kabla ya mradi kukamilika.
Diwani wa kata ya iwungilo regnadi danda amesema kuwa pamoja na mradi kuchelewa lakini pia baadhi ya vifa ikiwemo mabomba na saruji vimekuwa vikitolewa kijijini na kuuzwa mjini.
Mkandarasi wa maji katika halmashauri ya mji njombe jobu mwakasala amesema kuwa wananchi wanahaki ya kulalamikia mradi kuchelewa kutokana na serikali kushindwa kuwalipa wakandarasi kwa wakati sambamba na mkandarasi kufanya kazi chini ya kiwango.
Amesema kampuni iliyopewa tenda ya kutengeneza mradi huo imekwisha imaliza migogoro iliyokuwa inaendelea baina yake na sasa inaraji kuanza ujenzi baada ya serikali kupata fedha na kwamba mpaka sasa amekwisha lipwa milioni 600.
Post a Comment
Post a Comment