const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); HALMASHAURI NJOMBE NA IRINGA ZATAKIWA KUSIMAMIA UZALISHAJI KAHAWA - HABARI MPYA

..

HALMASHAURI NJOMBE NA IRINGA ZATAKIWA KUSIMAMIA UZALISHAJI KAHAWA

Post a Comment
Halmashauri za mikoa ya Njombe na Iringa zimetakiwa kuyafufua na kuanzisha mashamba mapya ya zao la kahawa kufuatia zao hilo ambalo limekuwa maarufu kwa kukuza uchumi miaka 80 kuanza kupuuzwa huku wakulima wake wakihamia katika kuzalisha mazao mengine.
Image result for njombe
Mkuu wa mkoa wa iringa amina masenza amesema kuwa hali ya uzalishaji wa zao hilo kwa mikoa ya njombe na iringa inazidi kushuka kila uchao na hivyo halmashauri zinatakiwa kushirikiana na bodi ya kahawa pamoja na kituo cha utafiti wa zao hilo TAKRI Ili kuhakikisha wakulima wengi wanajihusha kulima zao hilo la kahawa.

Meneja wa bodi ya kahawa kanda ya ruvuma na Iringa Peter Bubelwa anasema kuwa kilimo cha kahawa kinakabiliwa na changamoto kubwa ikiwemo wakulima kutotaka kutumia mbegu mpya na baadhi ya wakulima Kusalia wakiuza mazao nje ya mfumo wa vikundi .

Baadhi ya wakulima wamesema kuwa licha ya kuhamasika kulima zao hilo lakini wanakatishwa tama na hali ya kusekana kwa soko la uhakika ambalo linwafanya kuhamia katika kilimo cha mazao mengine.
NA PROSPER MFUGALE MAKAMBAKO

Related Posts

There is no other posts in this category.

Post a Comment