const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); Mama aliyemuuwa mwanawe naye afariki kwa Kutatanisha - HABARI MPYA

..

Mama aliyemuuwa mwanawe naye afariki kwa Kutatanisha

Mwanamke aliyekuwa akishikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kumuua mtoto wake katika kijiji cha wingwi micheweni pemba naye amefariki dunia huku polisi na hospitali wakitupiana mpira kuhusu mazingira ya kifo chake.

Jeshi la polisi ambao walikuwa wakimshikilia mwanamke huyo wamesema alifariki akiwa hospitalini lakini madaktari wamesema walipompokea mwanamke huyo kutoka kwa polisi akiwa tayari amefariki dunia.

Kamanda wa polisi mkoa wa kaskazini pemba Haji Khamisi Haji amesema waliamua kumpeleka hospitali mwanamke huyo baada kusema amebanwa na mafua ili ende kupatiwa matibabu .

Daktari aliyemfanyia uchunguzi marehemu huyo khalifan Said Salum amesema wamempokea mwanamke huyo kutoka kwa jeshi la polisi akiwa tayari ameshafariki dunia.
Amesema wakati anaendelea kumpima marehemu huyo walimkuta akiwa ametokwa na povu jingi mdomoni na hivyo kuchukuwa sampuli kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Hata hivyo mwandishi wa habari hizi akiwa anatoka katika hospitali ya micheweni amemuona mtuhumiwa wa pili wa tukio hilo akiwa anapelekwa hospitali kwa kupatiwa matibabu akiwa na ulinzi kutoka jeshi la polisi.
Marehemu pamoja na Watuhumiwa wenzake wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kumchinja Mtoto wao mchanga kama ilivyoripotiwa kwenye habari

Related Posts

Post a Comment