Mbali na kuwa kiungo muhimu katika mapishi, nyanya inaweza kutumika kama njia au dawa ya kupambana na mafuta katika ngozi ambayo kwa namna moja au nyingine husababisha kuharibika kwa ngozi hususan ya uso au kushambuliwa na chunusi.
Tatizo la mafuta katika uso limekuwa likiwakosesha raha wengi, na wamekuwa wakitafuta dawa ambazo huenda zikaongeza tatizo zaidi kutokana na kuwa na kemikali hatarishi kwa ngozi ya uso. Ili kuondokana na tatizo hilo unaweza kutumia nyanya kama njia salama ya kuondoa mafuta usoni.
Virutubisho vinavyopatikana katika tunda hili vikiwemo vitamini A vinasaidia kwa kiasi kikubwa kupambana na mafuta ya ziada ambayo hayatakiwi katika mwili.
Ili kuandaa nyaya kama dawa ya kuondoa mafuta ya ziada katika ngozi, fanya yafuatayo.
Anza kwa kukata nyanya katika vipande viwili, safisha uso wako kwa maji ya uvuguvugu kisha kausha kwa taulo au kitambaa safi.
Baada ya kuhakikisha uso umekuwa mkavu, chukua kipande cha nyanya na uanze kupaka taratibu katika uso, na uhakikishe majimaji yake yanabaki usoni.
Acha majimaji hayo yakae usoni kwa muda usiopungua dakika 20 kisha safisha tena uso kwa maji ya uvuguvugu.
Unaweza pia kusaga nyanya na kupata juisi yake ikiwa nzito ambayo itahitaji kuchanganywa kidogo na maji ya limao na kupata mchanganyiko ambao utasaidia kupunguza kama sio kuondoa kabisa mafuta katika ngozi ya uso.
Ili kupata matokeo mazuri, fanya hivi mara mbili kwa siku ndani ya mwezi mmoja, mabadiliko yataonekana katika ngozi yako na kuwa nyororo na kavu yenye mvuto.
Post a Comment
Post a Comment