Ndege ya shirika la wasamaria wema “Samaritan Purse’ international iliyowachukua watoto walionusurika katika ajali ya basi Karatu, katika uwanja wa Kilimanjaro International Airport (KIA) jana, imewasili Mjini Charlotte NC, nchini Marekani saa Moja iliyopita (majira ya saa 3 asubuhi, saa za Afrika ya Mashariki).
Watoto hao wamepelekwa moja kwa moja katika hospitali kuu mjini Charlotte kwa ajili ya kuimarishwa kiafya (medical stabilisation), na baadae watachukuliwa kwa ndege nyingine maalumu (air ambulance) kuelekea hospitali ya Mercy, Iliyopo Sioux City, katika Jimbo la Lowa kwa huduma kamili za matibabu.
Watoto hao waliondoka jana wakisindikizwa na wazazi wao, ambapo watakaa nchini Marekani kwa muda wote wa matibabu.
Aidha Mganga Mkuuwa Hospitali ya Mount Meru, Jackline Urio wakati wa kuwaaga watoto hao alisema kuwa kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia nchini Marekani, wanatarajia kuwa watoto hao watakuwa wamepona ndani ya miezi miwili na kurejea nchini kuendelea na masomo.
Post a Comment
Post a Comment