const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); WATAALAMU WAELEZA FAIDA ZA KUOGELEA UKIWA MTUPU - HABARI MPYA

..

WATAALAMU WAELEZA FAIDA ZA KUOGELEA UKIWA MTUPU

Kuogelea ni sehemu ya starehe kwa watu wengi na pia ni mazoezi kiafya. Watu wengi wamekuwa wakishiriki kuogelea kama sehemu ya kujifurahisha, na wengine hufanya kuogelea kama mchezo.

Watu wengi wamekuwa wakijiuliza maswali kama kuogelea kuna athari zozote kiafya. Wataalamu wa tiba na afya wametoa maoni yao kuhusu mjadala huo wa kuogelea ukiwa mtupu kabisa.

Dkt. Lance Brown wa Jijini Newyork marekani amefafanua kuwa “Kuvaa nguo za kujisitiri kunamuongezea jasho mwogeleaji na mtu kupata upele na muwasho. Ipe ngozi nafasi ya kupumua.”

Kwa mujibu wa wataalamu hao, kitendo cha kuwa mtupu kinaipa ngozi nafasi ya kupata vitamin D kirahisi.

Mshauri nasaha wa mambo ya jinsia, Shaun Galanos anasema kuwa ni suala ambalo linapendeza kuanzia chumbani, hadi juani katika mandari ya kuogelea.

“Kuwa mtupu si kwamba inakuongezea vitamin D pekee, hata hisia zako. Inasaidia hata mzunguko wako wa damu na kuondoa sumu mwilini.” 

Kwa mujibu wa watafiti wa Afya, mwili hupokea vitamin D kwa wingi unapoanikwa juani, walau kwa wastani wa kati ya dakika 10 hadi 15.

Dkt Jenn Mann anazungumzia mada hii kwa kusema kuwa watu wasiishie kuendekeza mlo tu, wakati kuna mbadala mzuri wa kuota jua.

“Kutumia muda wako ukiwa ‘mtupu’ juani ni namna ya kuwasiliana na mwili wako. watu wengi hivi sasa wanajiweka mbali na suala la kuupa hisia mwili, ambayo inaweza kumsaidia.”

Dkt Mann anaenda mbali zaidi, akiwashauri kinamama na ‘hasa wenye ngozi nyeupe’ kutumia njia hiyo kama mbadala wa kujipodoa, akiamini inawasaidia.

Kisaikolojia pia inaelezwa kuwa ni tendo linalomuondolea mtu hata hofu ya msongo wa mawazo unaotokea wakati huo na mtu anajihisi kuwa huru zaidi, akipigwa na upepo.

Pia inaelezwa kuwepo hoja kwamba wengi sasa wanaunga mkono mtazamo huo wa kuogelea kuwa watupu katika baadhi ya maeneo, ili kunufaika hivyo kiafya.
Wataalamu hawa wameejiuliza swali, Kwanini kuvaa nguo wakati unakwenda kujilowanisha majini?
Ngozi ambayo haijafunikwa na nguo hukauka haraka zaidi kuliko iliyofunikwa.
Vilevile inafafanuliwa kwamba kuogelea bila kuwa na mavazi, humuepusha mtu kutokana na muwasho unaoweza kusababishwa na mavazi ya kuogelea, humfanya mtu kuwa makini katika maeneo mbalimbali ya ngozi yake na kugundua kama kuna tofauti yoyote mwilini.

Kuogelea hukufanya kuwa mwepesi.

Wakati wa kuogelea ili songe mbele inakubidi kujikunja, kujivuta na kujisukuma ndani ya maji. Kufanya vitendo hivi mara nyingi kwa wakati mmoja kutakusaida kulainisha viungo vyako vya mwili. Hata kama huwa unafanya mazoezi ya viungo, jitahidi pia kuogelea mara kwa mara ili kuupa mwili wako wepesi wa viungo.

Kuogelea huongeza nguvu ya misuli yako.

Unapoogelea, misuli yote ya mwili huusishwa. Tofauti na wakimbiaji ambao wanahusisha zaidi misuli ya miguu. Ukiwa unaogelea unahusisha mikono kujivuta, miguu kujisukuma na tumbo hukaza ili kuipa miguu nguvu, hivyo kufanya kuogelea kuwa zoezi la kipekee linalohusisha viungo vingi mwilini.

Kuogelea hupunguza msongo wa mawazo.

Kuogelea ni mchezo unaofurahisha, unakufanya kupata utulivu wa ubongo na kukuburudisha. Baadhi ya wataalamu wamesema kuwa unapoogelea ubongo wako huachana na fikra nyingine zote na kutulia ili kukufanya uogelee pasipo kuwa na matatizo. Hivyo kama unajisikia mchovu na mwenye msongo wa mawazo, basi ni wakati mzuri wa wewe kwenda kuogelea.

Kuogelea ni tiba ya ngozi.

Kwa wale wenye matatizo ya kuwa na ngozi kavu au muwasho katika mwili, kuogelea katika maji ya chumvi (baharini) kuataitibu ngozi yako. Chumvi iliyoko katika maji ya bahari itaifanya ngozi kuwa yenye unyevunyevu na kurudisha seli zilizokufa. Utashangaa namna ngozi yako itakavyokuwa nyororo mara baada ya kutoka kuogelea katika maji ya bahari.

Swali la kujiuliza hapa pamoja na faida zote zilizoelezwa na wataalamu, Je utamaduni wetu wa kiafrika unalionaje suala hili?

Related Posts

2 comments

Post a Comment