Hatimaye kundi la vichekesho lililojipatia umaarufu mkubwa nchini la Orijino Komedi, limefikia mwisho kwa kusambaratika, huku chanzo kikidaiwa kuwa ni mmoja wa memba wake mwenye mbwembwe nyingi, Silvery Mujuni, maarufu kama Mpoki a.k.a Mwarabu wa Dubai, Risasi Mchanganyiko limenyetishiwa.
Kwa mujibu wa chanzo kilicho karibu na kundi hilo ambalo halijarusha kazi zake hewani kwa muda mrefu sasa, limeingia katika hatua hiyo, baada ya mmoja wa memba wake, kukiuka makubaliano, kitu kilichosababisha wote waamue kufanya mambo kivyao.Inadaiwa kuwa hapo awali, kulikuwa na maazimio ya kila mmoja kuleta kundini, makubaliano yoyote ya kazi kibiashara ili mapato yatakayopatikana, wagawane wote.
“Walijua kuwa kazi zao kama kundi ziliwavutia kampuni na mashirika, lakini wakafahamu pia kuwa wakati mwingine siyo rahisi kundi kuingia mikataba, kwamba wapo ambao wangeweza kuvutiwa na mmoja wao, hivyo ikitokea namna hiyo, basi aliyepata dili hilo, alilete kundini, ambako yeye atapewa asilimia kubwa, huku wenzake nao wakipata kidogokidogo,” kilisema chanzo hicho.
Post a Comment
Post a Comment