Jeshi la polisi na idara ya uhamiaji kwa kushirikiana na wananchi wamefanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu 15 raia wa Ethiopia waliokuwa wakisafiri kwenda Afrika Kusini ambapo wamekutwa wakiwa wamefichwa kwenye shamba la mahindi katika kijiji cha Ipumpila wilayani Momba mkoani Songwe.
Wananchi wa kata ya Ndalambo ndio waliobaini kuwepo kwa wahamiaji haramu.
Afisa uhamiaji mkoa wa Songwe Elizeus Mshongi amesema tukio hilo linatokea wakati ambapo tayari raia wengine watano wa Ethiopia wameshakamatwa wakahukumiwa ,na kwamba changamoto kubwa iliyopo ni wahamiaji haramu hao kusaidiwa na watanzania wanaojua njia za maficho na kuongeza kuwa watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani jumatatu hii kukabiliana na mkono wa sheria.
Post a Comment
Post a Comment