Kocha wa klabu ya Eldense, Filippo Vito di Pierro na mkurugenzi mtendaji wa klabu hiyo Nobile Capuani wamekataa kuwa walihusika na shutuma ambazo zimewekwa dhidi yao kuhusiana na upangaji matokeo huku wakilaumu klabu ya Barcelona B kwa kukataa kuacha kufunga walipopoteza kwa mabao12-0.
Watu hawa wawili walikuwa miongoni mwa watu watano ambao walikamatwa na polisi wa usalama wa raia na makosa ya jinai huko Hispania baada ya matokeo hayo mabovu ya daraja la tatu.
Waliachiwa siku ya Jumatano lakini wana kesi za kujibu dhidi yao ambazo zinahusu rushwa baina ya watu na kujihusisha na makundi ya kihalifu.
Akihojiwa kuhusiana na tuhuma hizi na kama kwa namna yoyote wamehusika na wanafahamu lilitokea kwenye upande wa Eldense na upangaji matokeo, Di Pierro alisema “hakuna ukweli wowote na haijatokea.”
“Baada ya udhalilishaji huo kutokana na matokeo ya siku ya Jumamosi naamini kuwa wachezaji wetu wote 20 ni wasafi katika hili.”
“Wachezaji wa Barcelona hawakuheshimu kanuni ya utu na busara baiana ya timu hizi. Kiukweli wachezaji wetu katika benchi waliomba Barcelona isiendelee kufunga na wachezaji wa Barcelona waliweza kujibu kwa kusema tu “Samahani hatuwezi kuacha.”
Akikataa kujihusisha na suala lolote la upangaji matokeo, alisema: “Hii ni moja tu ya zile ndoto mbaya.
“Sielewi wanazungumzia nini kwakweli, sio sehemu ya nilivyo na sipo hivyo. Nitakuwepo kusaidia vyombo na mamlaka husika kwa namna yoyote nitakayoweza.”
Post a Comment
Post a Comment