Kila mshabiki wa soka akiulizwa kuhusu yupi mshambuliaji hatari zaidi Uingereza baasi jina la Romelu Lukaku, Diego Costa, Zlatan Ibrahimovich na Alexis Sanchez ni lazima yatakuwepo miongoni mwa majina yatakayotajwa.
Lakini sivyo, takwimu zinaonesha washambuliaji hao wako juu tu kutokana na muda mrefu wanaopewa uwanjani na pia kutokana na mipira ya adhabu kama faulu na penati ndio vinawaweka juu sana.
Lakini Olivier Giroud ni hatari zaidi yao, takwimu hazidanganyi. Takwimu zinaonesha Olivier Giroud ndio mshambuliaji ambaye hutumia dakika chache zaidi kucheka na nyavu kwani magoli yake 9 ameyafunga kwa kila baada ya dakika 88.11 alizokuwa uwanjani.
Wakati kinara wa magoli EPL Romelu Lukaku ametumia dakika 125.57 kwa kila goli alilofunga, hii inamaanisha Lukaku anatumia muda mwingi sana kuweza kufunga tofauti na Giroud ambaye humchukua dakika chache tu kucheka na nyavu.
Pengine Giroud angepewa nafasi na dakika sawa za uchezaji kama Lukaku ingekua sasa amempita Mbelgiji huyo kimagoli, Harry Kane yuko nafasi ya pili ya washambuliaji ambao hutumia dakika chache zaidi kucheka na nyavu huku yeye akitumia dakika 99.68.
Sergio Kun Aguero naye yumo katika nafasi ya tatu huku yeye hutumia dakika 124.8 kwa kila goli alilofunga, Lukaku yuko nafasi ya nne lakini chini yake yupo Alexis Sanchez ambaye naye hutumia dakika 136.06 kwa kila goli alilofunga msimu huu.
Zlatan Ibrahimovich yeye hutumia dakika 146.25 kwa kila goli alilofunga, na nafasi ya 6 yuko mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa ambaye yeye hutumia dakika 146.29 kwa kila goli alilofunga msimu huu.
Post a Comment
Post a Comment