Kipindi ni kipindi ambacho mengi yanazungumzwa na ambayo pia hayatofika kikomo mpaka pale ambapo dirisha la usajili litakapofunguliwa. Ni kipindi ambacho tetesi kadhaa zimeendelea kushika kasi na Alexis Sanchez ameendelea kuwa sehemu ya hili.
Baada ya kuwa katika kipindi kigumu na ambacho anaonekana kutokelewana na kocha wake Arsene Wenger huku pia akionekana kutokuwa tayari kusaini mkataba mpya kutokana na kutokuelewa mwenendo wa klabu hiyo, na mipango ya muda mrefu.
Na pamoja na kunukuliwa akisema anafurahia maisha ya London nyota wa klabu ya Arsenal Alex Sanchez amepokea simu ya kocha Jose Mourinho akitakiwa kujiunga na klabu ya Manchester united .
Taarifa zinasema kuwa Sanchez ni moja ya nyota wanaohitajika na mourinho kwa ajili ya kuimarisha kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao.
Televisheni ya Chile kupitia kipindi cha ‘El Show de Prensafutbol” imeripoti kuwa kocha huyo wa Manchester United alimpigia simu mchezaji huyo kumshawishi ajiunge na klabu ya Manchester United msimu ujao. TV hiyo pia imeweka wazi kuwa hata Pep Guardiola amekuwa akijaribu kumfikia Sanchez kwa kutaka atue City.
Hata hivyo kutokana na tetesi za Hazard kuelekea Sanatiago Bernabeu, klabu ya Chelsea inaonekana kuwa mstari wa mbele na pia taarifa zinadai kuwa imeshafanya nae mazungumzo.
Post a Comment
Post a Comment