Inawezekana mchezaji James Rodriguez akawa ni dhahabu kwa vilabu vingine ambavyo bado vinampa nafasi na vinamhesabu kuwa mchezaji bora hasa kwa nafasi yake, lakini kwa Real Madrid anaonekana kuendelea kuwa mchezaji ambaye njia yake ya kutokea ipo wapi.
Baada ya uvumilivu wa muda mrefu hatimaye kiungo James Rodriguez wa Real Madrid ameanza kuonesha hisia zake za kutofurahia maisha katika timu hiyo baada ya kupiga ngumi benchi kufuatia kufanyiwa mabadiliko katika dakika ya 72 kwenye mchezo dhid ya Leganes.
Katika mchezo huo ambao Madrid walipata ushindi wa mabao 4 kwa 2 James alifunga bao moja na kutoa pasi maridhawa ya goli la nne lakini furaha ya nyota huyo iliisha baada ya kuona dalili za kufanyiwa mabadiliko.
Kocha Zinedine Zidane amesema ni kawaida kwa mchezaji kutofurahia kutoka kwani kila mchezaji hutamani kucheza dakika tisini. Tukio hilo limechochea kuongezeka kwa taarifa zinazomuhusisha mchezaji huyo raia wa Colombia huyo kuihama Real Madrid mwishoni mwa simu huu.
Vilabu vingi vimeendelea kuhusishwa na James Rodriguez huku vilabu vya ligi kuu ya Uingereza vikionekana kumtolea macho zaidi hsa Chelsea, Liverpool pamoja na Arsenal wakionekana kuwa mstari wa mbele huku Bayern Munich ikitajwa kuwa klabu inayomvutia zaidi.
Post a Comment
Post a Comment