const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); PROFESA UDSM ALAANI NAPE KUWAKANYAGA WAMAMA, NAPE AMJIBU HIVI - HABARI MPYA

..

PROFESA UDSM ALAANI NAPE KUWAKANYAGA WAMAMA, NAPE AMJIBU HIVI

Ikiwa ni siku moja tu baada ya Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Mtwara kupitia tiketi ya CCM, Mhe. Nape Nnauye kulakiwa kimila na baadhi ya wafuasi wake wakiwemo akinamama walioonekana kulala chini na kisha Mbunge huyo ambaye kwa sasa ameendelea kujihimalisha zaidi kwenye medani za kisiasa za ‘kipekee’ baada ya kuondolewa Uwaziri wa Serikali ya awamu ya tano, ameibuka na kumjibu Profesa Issa Shivji kufuatia tukio hilo ambalo Prof. Shivji alitoa ushahuri.


Kupitia ukurasa wa twitter wa Prof. Shivji majira ya jioni alibandika picha ya Nape akionekana kupita juu ya Wanawake hao waliokuwa wakimlaki kimila na kuandika: Angekataa. ‘Nawashukuru sana mama zangu. Nilijitolea kuwahudumia, kuwa chini yenu kama mtoto wenu, sio kuwakanyaga’.
Hata hivyo baada ya andiko hilo la Profesa Shivji, watu mbalimbali walipata kutoa maoni yao kuhusiana na tukio hilo ikiwemo mila na tamaduni za Mtanzania ambazo zipo toka enzi. (tazama picha chini). Lakini baada ya kupita saa moja tokea kuweka andiko hilo, Nape kupitia kurasa wake wa twitter aliweza kumjibu Profesa Shivji, ambapo aliandika: Kwa mila za kusini tendo hili ni la heshima KIMILA na ukikataa ni sawa na DHARAU KUBWA kwa waliokufanyia, hata hivyo ndio maana NILILIZWA!.
Hata hivyo MO Blog imeshuhudia mjadala huo ukipamba moto hasa kupitia mitandao ya kijamii kwa kila mmoja akijadili jambo hilo kwa namna anavyojua yeye juu ya mila hizo.


Related Posts

Post a Comment