Baada ya ukimya wa miaka kadhaa na misukosuko aliyopitia, Ray C ameweka wazi mpango wake wa kuyateka tena mawimbi ya radio na vituo vya runinga kwa kuachia mzigo wenye ujazo kamili.
Mwimbaji huyo ambaye tangu mwaka jana alikuwa akipost picha kadhaa kwenye mitandao ya kijamii akiwa studio, amefunguka kupitia Twenzetu ya 100.5 Times Fm kuwa tayari ameshapika nyimbo nane ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya albam yake.
Hata hivyo, Ray C amedai kuwa hajaridhika na nyimbo zote alizofanya hivyo ataendelea kurekodi kabla ya kuanza kurusha makombora mfululizo yakifuatiwa na albam hiyo.
“Hata hivyo bado sijaridhika ni nyimbo gani nitoe kwa sababu bado nilizokuwa nazo sijaridhika kwa sababu nimekulia katika maisha ya kutoa nyimbo kumi au kumi na tano halafu ndio natoa wimbo mmoja [kwanza], sijazoea kurekodi wimbo mmoja halafu nikaharakisha kutoa,” alisema Ray C.
Aliongeza kuwa anachofanya ni kuhakikisha anapata nyimbo tano bora zaidi zitakazochuana kila atakapokuwa akiziachia na kwamba kila siku anapoingia studio hujikuta akirekodi wimbo mkali zaidi ya uliopita, ndio sababu ya kutaka kuongeza nyingine.
‘Kiuno Bila Mfupa’ alidai kuwa anatarajia kuiza albam yake na kuiuza duniani kote kupitia mtandao.
Hivi karibuni, Ray C aliwaonjesha mashabiki wake ladha ya sauti yake kwa kurudia wimbo wa Recho ‘Upepo’ na kudhihirisha kuwa bado ana uwezo mkubwa.
Post a Comment
Post a Comment