const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); Wananchi waandamana na Maiti Kahama, Wachimba Kaburi Ofisini kwa Diwani - HABARI MPYA

..

Wananchi waandamana na Maiti Kahama, Wachimba Kaburi Ofisini kwa Diwani

Kahama. 
Wananchi wa Kata ya Mhongolo mjini hapa jana waliandamana bila kibali wakiwa na jeneza la mtoto aliyefariki mtaani hapo kwa lengo la kwenda kuuzika mwili huo kwenye Ofisi ya kata hiyo wakidai diwani wa kata hiyo, Michael Mizubo ameuza eneo la makaburi kwa maslahi yake binafsi.
Mmoja wa wananchi hao aliyejulikana kwa jina moja la Paulina ambaye alikuwa akiongoza maandamano hayo, amesema waliamua kwenda kuzika mwili huo wa mtoto huyo aliyejulikana kwa jina moja la Rosemary aliyefariki kwa ugojwa wa kawaida kwenye ofisi hiyo ya kata, kwa sababu hakuna eneo la kuzika.

Hata hivyo wakati wanachimba kaburi hilo kwenye mlango wa ofisi ya diwani huyo kwa lengo la kuuzika mwili huo polisi walifika na kuwatawanya kwenye eneo hilo kwa madai ni ukiukwaji wa taratibu.

Kwa upande wake diwani wa kata hiyo Mizubo anayedaiwa kuuza eneo la maziko amesema wananchi hao walikuwa na sababu zao za kisiasa kwani pamoja na eneo hilo la makaburi kuuzwa tayari kuna eneo jingine limetengwa kwa ajili ya maziko hayo.


DOWNLOAD APPS YA TZTOWN HAPA

http://www.androidcreator.com/apk/app221302.apk
WANANCHI WAOMBA SERIKALI KUODOA TAKA KIZIMBANI MAKAMBAKO MKOANI NJOMBE


Related Posts

Post a Comment