const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); Achomwa Moto pamoja na Pikipiki Wilayani Chunya - HABARI MPYA

..

Achomwa Moto pamoja na Pikipiki Wilayani Chunya

Mtu mmoja jinsi ya kiume ambaye hajafahamika jina,umri wala makazi mwili wake umekutwa umeuawa kwa kuchomwa moto na mtu au watu wasiofahamika kilometa saba kutoka kijiji cha Ifumbo kitongoji cha mwabangala eneo la Iponda Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya. 
Wakithibitisha kutokea kwa tukio hilo Mwenyekiti wa kijiji cha Ifumbo Lyashi Mwambyalo na Kaimu mtendaji wa kijiji cha Ifumbo Emili Rajab wamesema walipata taarifa kutoka kwa wananchi majira ya saa moja asubuhi ambapo walifika eneo la tukio na kukuta mwili umeteketezwa kwa moto pembeni kukiwa na pikipiki ambayo nayo iliteketezwa kwa moto.

Uchunguzi wa awali unaonesha kuwa eneo la tukio hilo kuna nyayo za mifugo inayodhaniwa kuwa ni ng’ombe lakini haikuwepo kwa wakati huo. 

Aidha baada ya kushuhudia Kaimu mtendaji Emili alitoa taarifa kituo cha Polisi Chunya ambapo walifika eneo la tukio wakiwa na Madaktari ambao waliufanyia uchunguzi mwili wa marehemu na kisha kuamuru uzikwe kutokana na kuharibika vibaya na mabaki ya pikipiki yalichukuliwa kwenda kituo cha Polisi Chunya kwa uchunguzi zaidi.

Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Chunya Rehema Madusa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba wanachi waache tabia za kujichukulia sheria mkononi . 

Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Dhahiri Kidavashari amekiri kuwepo kwa tukio hilo na kuwataka wananchi kuacha tabia za kujichukulia sheria mkononi na huenda tukio hilo linahusishwa na uzoefu wa matukio ya uhalifu hivyo wananchi kuchoshwa na vitendo hivyo. 

Hata hivyo ameonya kuwa mhalifu anapokamatwa afikishwe kwenye vyombo vya sheria ili sheria ichukue mkondo wake. 

Aidha Jeshi la Polisi linafanya uchunguzi zaidi na tukio hilo ili kubaini wahusika na ikithibitika wafikishwe mahakamani pindi upelelezi utakapokamilika.


DOWNLOAD APPS YA TZTOWN HAPA

http://www.androidcreator.com/apk/app221302.apk
WANANCHI WAOMBA SERIKALI KUODOA TAKA KIZIMBANI MAKAMBAKO MKOANI NJOMBE


Related Posts

Post a Comment