const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); - HABARI MPYA

..

Hakuna mtumiaji wa simu janja duniani asiyetumia programu tumishi (apps) katika simu yake na hii ni kwa sababu tunahitaji programu tumishi ili kuweza kutumia simu zetu vizuri zaidi.
Katika taarifa zilizotoka hivi karibuni katika mitandao kama vile Telegram, Amnesty International zimetoa takwimu kuhusiana na programu tumishi zilizo na ulinzi zaidi kwa mwaka 2016. Lakini unaweza ukawa unajiuliza Programu tumishi ni nini?

Programu tumishi au apps kama wengi wetu tulizoea ni programu fulani unaweza kutumia kwenye simu au kompyuta katika kufanikisha jambo fulani.

Mfano wa apps ni Facebook Messenger, WhatsApp, Gmail, GDrive, n.k.
Orodha ya programu tumishi/apps zilizo na usalama zaidi kulingana na kampuni inayoimiliki/inayozimiliki

Facebook

Facebook inamiliki programu tumishi mbili; WhatsApp na Facebbok Messenger. WhatsApp ambayo hivi sasa inashikilia namba moja kwa kuwa app ambayo ina ulinzi wa kutosha; mazungumzo baaina ya mtu na mtu au mazunguzo ya kwenye group yanabaki kuwa kati yenu wawili.

WhatsApp na FB Messenger zote zinamilikwa na Facebook.

Facebook Messenger si salama sana kwa sababu yenyewe haina feature ijulikanayo kama end-to-end encryption. Apps hizi 2 kwa ujumla zina watumiaji zaidi ya bil. 2. 

Ilipata kura 73/100

Apple

Kampuni hii yenye kumiliki iMessage na Facetime yenyewe imeshika nafasi ya pili katiaka orodha ya apps zenye uinzi wa kuaminika kwani apps hizo 2 haziwezi kuonyesha taarifa kwa mtu asiyehusika (iwapo app ikidukuliwa) hakuna atakayeweza kuelewa isipokuwa Apple wenyewe. Hata hivyo apps hizi zimetakiwa kuwaeleza watumiaji wote ni muda taarifa zao zinakuwa salama na ni wakati hazipo salama mathalani iwa mtu atatuma ujumbe kwenda kwa mtu asiyetumia iPhone.

Ilipata kura 67/100

Apple wameweka wazi kuwa wenyewe watatoa.

Telegram

Telgram in app ambayo ilikuwa ya kwanza kuwezesha watu kutuma nyaraka katika mfumo wa “.doc” kabla ya app nyingine yoyote kuiga kitu hicho. Cha kushangaza ni kwamba Telegram ile feature ya ‘end-to-end encryption’ sio ya papo kwa papo (default); huwezi kujua ni wakati gani taarifa zalo zipo salama.

Ilipata kura 67/100

Telegram inawatumiaji wa mara kwa mara takribani 100 milioni kila mwezi

Google

Google ambao ni wamiliki wa programu tumishi Allo, Duo na Hangouts. Ukiwa na Allo app basi mawasilisno yataabaki kuwa baina yenu mnaowasiliana tu huku kwenye Duo ni chagua lako kukubali end-to-end encryption au kukataa. Hangouts haina end-to-end encryption kwahiyo si salamasana kwani taarifa zako hazijafichwa.

Tazama video Mtoto amvua kofia Papa Francis

Related Posts

Post a Comment