ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amemtembelea Mshauri wa Kampuni ya Quality Group, Yusuph Manji aliyelazwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).
Manji ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mbagala Kuu, alifikishwa kwenye taasisi hiyo Febuari 12 akitoka Polisi kutokana na maradhi yanayomsumbua.

Manji alifika Kituo Kikuu cha Polisi Febuari 9 kuitika agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa kile kinachodaiwa kuhusika na dawa za kulevya.
Akizungumza na Gazeti hili jana Dar es Salaam, baada ya kumjulia hali Manji, Gwajima alisema alimwombea na anaendelea vizuri.
“Nimetoka kumwangalia na kumjulia hali Manji, nimemwombea sala fupi, lakini anaendelea vizuri,” alisema Gwajima.
Gwajima ni miongoni mwa watu waliotajwa na Makonda akidaiwa kujihusisha na dawa za kulevya na alishikiliwa na Polisi na ndiko walikutana na Manji.
Gwajima alitoka Polisi Febuari 11 huku Manji akiendelea kushikiliwa hadi alipopata maradhi ghafla na kupelekwa hospitali.
Februari 12, Gwajima alikaririwa na gazeti hili akisema hadi alipoachwa kutoka kituoni hapo Manji alikuwa bado anashikiliwa.
“Sioni sababu ya kuendelea kushikilia watu wale bila hatua, kama mimi nilituhumiwa tena kwa kutangazwa, lakini mwishowe ikabainika hakuna ukweli, nitaamini vipi kama waliobaki ndani mikononi mwa Polisi nao wanahusika?” Alihoji.
KAMA ULIMIS VIDEO YA MCHEZAJI WA Ghana ALIE JIKANYAGA KWA KUWASHUKURU MUKE NA MCHEPUKO WAKE TAZAMA HAPA
Post a Comment
Post a Comment