const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); Agness Gerald (Masogange) acheleweshwa na foleni Jangwani, kesi yaendelea - HABARI MPYA

..

Agness Gerald (Masogange) acheleweshwa na foleni Jangwani, kesi yaendelea

Upelelezi wa kesi ya kutumia dawa za kulevya inayomkabili Msanii Agnes Gerald maarufu kama Masogange (28) katika Mahakama ya Kisutu bado haujakamilika na imeahirishwa, 
huku akishindwa kufika mahakamani hapo kutokana na kukwama kwenye foleni. 
Image result for Masogange
Wakili wa Serikali, Adolf Mkini aliyaeleza hayo leo wakati kesi ilipotajwa kwa Hakimu Mkazi Mkuu, 
Wilbroad Mashauri. 

Mkini alidai kuwa upelelezi bado haujakamilika na mshtakiwa hayupo mahakamani hapo. Baada ya kueleza hayo, wakili wa Masogange, 
Nictogen Itege ameiarifu Mahakama kuwa mteja wako hiyo alikuwa njiani kuelekea mahakamani lakini alikwama katika foleni eneo la Jangwani.

Kesi imeahirishwa hadi Aprili 20, 2017 kwa ajili ya kutajwa ili kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika ama la. Masogange anakabiliwa na mashtaka mawili ya kutumia dawa za kulevya aina ya Heroin na Oxazepam.

KAMA ULIMIS VIDEO YA MCHEZAJI WA Ghana  ALIE JIKANYAGA KWA KUWASHUKURU MUKE NA MCHEPUKO WAKE TAZAMA HAPA


Related Posts

Post a Comment