JOHN Stephen
Akhwari. Ni jina la
mwanariadha mkongwe
wa Tanzania mwenye
rekodi ya kipekee katika kumbukumbu za kimataifa za mchezo huo. Mwaka 1968 katika mbio za Olimpiki
kule Mexico, alipewa tuzo ya aina yake kutokana na tukio la ajabu alilolifanya.
Mbio zilishaisha muda mwingi tu, hata sherehe za kugawa medali zilimalizika pia, kila mtu akajua mambo
yameisha na watu wakaanza kutoka uwanjani. Kwa mbali zikaonekana pikipiki za eskoti zinamsindikiza mtu
anayekuja akitembea huku damu zikimvuja miguuni baada ya kuumia akiwa mbioni, alikuwa ni Akhwari.
Alipoulizwa kulikoni, alisema licha ya kuumia kwake kulikomfanya ashindwe kuendelea kukimbia,
amelazimika kukataa kusikiliza ushauri wa kujitoa, hivyo kutembea mpaka kufika uwanjani hapo ili aweze
kutimiza kile alichotumwa na nchi yake, yaani kumaliza mbio.
Dunia nzima ikamshangaa, wazungu wanavyojua kuthamini, hiyo ikawa rekodi inayoheshimika kimataifa
mpaka leo na kuna tuzo imepewa jina lake ikiheshimu ari na moyo wa kujituma bila kukata tamaa.
Achana na hilo.
Akhwari anayo stori nyingine kali isiyofahamika. Inahusu kuyeyuka kwa Scania zake mbili,
unajua ilikuwaje?
TUMJUE KWANZA AKHWARI NI NANI
Alizaliwa mwaka 1938 wilayani Mbulu, Manyara akiwa ni mtoto wa saba kati ya watoto 18 wa familia ya
mzee Stephen Akhwari aliyekuwa Mwalimu wa Dini katika Kanisa Katoliki. Mama yake aliitwa Veronica
Qamara.
Riadha kwake amezaliwa nayo. Alianza mbio tangu utotoni hasa alipokuwa Darasa la Tatu katika Shule ya
Endagikot. Hadi anamaliza Darasa la Nane (enzi za mkoloni) mwaka 1958,
alishakuwa mahiri katika mchezo
huo.
Ni mwanariadha wa kwanza Mtanzania kushiriki mashindano ya kimataifa baada ya kukimbia katika mbio za
Afrika Mashariki zilizotimka Kenya mwaka 1962, huko alipata tiketi ya kushiriki mashindano ya Jumuiya ya
Madola yaliyofanyika katika jijini Perth, Australia baadaye mwaka huo na kufanikiwa kushika namba sita.
Pia aliwahi kuzawadiwa soda katika mbio za Siku ya Malkia wa Uingereza enzi hizo za ukoloni.
“Nilikuwa bado mdogo, nilishindana na wakubwa na nikawa mtu wa 40, Bruce Ronaldson (aliyekuwa Mkuu
wa Wilaya ya Mbulu), akanizawadia soda ya Coca Cola maana nilikuwa mshiriki pekee mwenye umri mdogo.
Enzi zile za ukoloni Mwafrika kunywa soda lilikuwa ni jambo lisilowezekana,” anasema.
KAMA ULIMIS VIDEO YA MCHEZAJI WA Ghana ALIE JIKANYAGA KWA KUWASHUKURU MUKE NA MCHEPUKO WAKE TAZAMA HAPA
Post a Comment
Post a Comment