Gari la Mbunge wa Tarime Mjini Mh.Ester Matiko (Chadema) limepata ajali na kusababisha KIFO cha mwendesha boda boda papo hapo.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo amesema limetokea maeneo ya Magu-Mwanza wakati ambapo mbunge huyo akiwa njiani kuelekea Tarime ndipo alipomgonga Mwendesha pikipiki ambaye bado jina lake halijafahamika
Imeelezwa kuwa Mbunge huyo ameumia sehemu kadhaa za mwili wake.
"Ahsante mdogo wangu nimepata ajali mbaya sana ila Mungu ameona niendelee kuishi".Ujumbe ambao Ester Matiko aliomwandikia kada wa Chadema Mhere Mwita mbapo alitoka kumjulia hali
Chanzo; Faharinews
ANGALIA VIDEO CHIDEO
Post a Comment
Post a Comment