const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); MKUU WA MKOA LINDI ASITISHA UHAMISHO WA WATUMISHI WA KITUO CHA AFYA TINGI - HABARI MPYA

..

MKUU WA MKOA LINDI ASITISHA UHAMISHO WA WATUMISHI WA KITUO CHA AFYA TINGI




Mkuu wa mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi amesitisha uhamisho wa watumishi wa nne kati ya watano waliotakiwa kuhama kutoka kwenye kituo cha afya cha Tingi wilaya ya Kilwa.

Zambi alisitisha uhamisho huo juzi alipokuwa anazungumza na wananchi wa kata ya Tingi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Tingi.

Mkuu huyo wa mkoa ambae kabla ya kutoa uamuzi huo alisikiliza maelezo ya wananchi, baadhi ya waguuzi, mganga kiongozi wa kituo hicho na baadhi ya wakuu wa idara wa halmashauri ya wilaya hiyo. 

Alisema kutokana na utata wasababu zilizoelezwa kuhusu uhamisho huo na mazingira yaliyosababisha kifo cha mtoto wa miaka tisa aliyefia katika kituo hicho mwanzoni mwa mwezi uliopita, aliamua kusitisha uhamisho wa watumishi wanne kati ya watano waliopewa barua za uhamisho hadi yapatikane matokeo ya uchunguzi utakaofanywa na tume maalumu itayoundwa na ofisi yake hivi karibuni.

Alisema pamoja sababu zilizotolewa na mganga mkuu wa hosipitali ya wilaya ya Kilwa, Dkt Vitalis Katalyeba kuhusu uhamisho huo lakini ameona kuna haja ya kusitisha ili uchunguzi wa kina ufanyike.
"Pamoja na sababu zilizo elezwa lakini bado uchunguzi unahitajika, kituo hiki kina watumishi 22 sawa na kituo cha Masoko ambacho kipo karibu na hosipitali ya wilaya, kinahudumia watu wengi kuliko kituo cha Masoko. Lakini wamehamishwa watumishi watano wakati Masoko wamehamishwa wawili tu, hata hivyo uhamisho unafanyika kukiwa ni muda mfupi tangu kuibuliwa tatizo la umeme na yanayotokea baada ya kuelezwa tatizo hilo, wananchi hawa nirahisi kuamini kuwa umetokana na sababu hiyo,"alisema Zambi.

Kuhusu mazingira ya kifo cha mtoto, mkuu wa mkoa Zambi alisema kuna utata mkubwa wamaelezo uliosababisha kuhitajika uchunguzi wa kina. Alibainisha kwamba japokuwa maelezo ya mlezi wa mtoto aliyefariki, Magreth Nguli, kwakiasi kikubwa yalifafana na ya muuguzi Mwanaisha Amanzi kuhusu muda aliofariki mtoto huyo, muda ambao alifikishwa katika kituo hicho kutoka katika zahanati ya Miteja, muda muuguzi Mwanaisha aliomba gari kwa mganga mkuu wa wilaya kwa ajili ya kumkimbiza hosipitali na muda ambao gari hiyo ilifika katika kituo hicho wakati mtoto huyo amefariki.

Lakini maelezo ya mganga mkuu yalitofautiana na maelezo ya Mwanaisha na Magreth. Huku baadhi ya fomu za taarifa zilizoandikwa kituoni hapo zikiwa zimebadilishwa maelezo ya taarifa zikiwa na miandiko ya watu zaidi ya wawili.

Sambamba na uamuzi wa kusitisha uhamisho huo, Zambi ambae pia nimwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa, alimvua madaraka mganga kiongozi wa kituo hicho, ofisa tabibu Christopher Kunde. Huku akimuagiza mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo, Zabron Bugingo ambae alikuwepo mkutanoni hapo, amuhamishe kutoka katika kituo hicho.

Kutokana na kuchelewa kuandaa taarifa muhimu za kifo cha mtoto huyo kwa takribani majuma mawili tangu kutokea kifo hicho. Tena ni baada ya mkuu wa wilaya hiyo Christopher Ngubiagai kwenda kituoni hapo na kuelezwa kuwa pamoja na sababu nyingine kifo cha mtoto huyo kilichangiwa na kitendo cha kutopelekwa gari haraka.

Awali muuguzi Mwanaisha ambae kwakiasi kikubwa maelezo yake yaliungwa mkono na mlezi wa mtoto huyo alisema mtoto huyo alifikishwa kituoni hapo saa nne asubuhi na ndio muda ambao alimpigia simu mganga mkuu wa wilaya kumuomba gari hata hivyo hakupata ushirikiano kutokana na kilichoelezwa kutokuwa na mahusiano mazuri baina yao.
"Nilimpigia simu saa kwenye saa nne, badala ya kumuambia alisema mimi sikupaswa kumuomba. Bali muuguzi wa zahanati ya Miteja huku akinilaumu kwanini nilimueleza mkuu wa wilaya na waandishi wa habari tatizo la umeme." aliniuliza mgonjwa alikuwa na umri gani nilipomtajia alikata simu na kuacha kabisa kupokea simu nilizokuwa na mpigia hadi nilipotumia simu ya mmoja wa ndugu za mgonjwa," Alisema Mwanaisha.

Kwa upande wake dkt Katalyeba ambae maelezo yake kuhusu sababu za uhamisho wa wawatumishi hao yaliungwa mkono na katibu wa bodi ya afya ya hosipitali ya wilaya, John Maongezi. Alisema uhamisho huo ulikuwa wa kawaida kutokana na upungufu mkubwa watumishi wa idara ya afya wilayani humo, kiasi cha kusababisha baadhi ya zahanati kuwa na muuguzi mmoja.
"Uhamisho huu haujalenga kituo cha Tingi pekee yake bali hata vituo vingine watumishi wake wamehamishwa na hakuna sababu nyingine zaidi ya hiyo," alisema Dr Katalyeba.

Kuhusu kuchelewa kupelekwa gari na muda gari hiyo ilipofika katika kituo cha Tingi. Mganga mkuu huyo alisema "Taarifa ilinifikia saa sita na nusu, aliyenipigia simkumbuki maana nilikuwa naendelea nakazi ya upasuaji, hata simu niliwekewa sikoni na mtu, na gari hiyo ilifika saa nane na nusu mchana katika kituo hiki," alisema Dr Katelyeba.

Mwanzoni wa mwezi uliopita, mkuu wa wilaya hiyo, Christopher Ngubiagai alikwenda katika katika kituo hicho nakuambiwa kuwepo changamoto ya umeme na maji.

Ambapo pia alikwenda mwishoni mwa mwezi kuona utekelezaji wa agizo lake kwa shirika la umeme (TANESCO) kuhusu kushugulikia tatizo la umeme katika kituo hicho.

Ndipo alipoelezwa kuwa pamoja na tatizo la umeme kushugulikiwa kikamilifu na kumalizwa. Lakini ziara yake na maagizo aliyotoa yalisababisha kujenga uhasama baina ya muelezaji wa tatizo hilo la umeme (Mwanaisha Amanzi) na mganga mkuu wa hosipitali ya wilaya (Dr Vitalis Katalyeba).

Related Posts

Post a Comment