const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); MATUKIO MBALIMBALI KUHUSU WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO BUNGENI MJINI DODOMA - HABARI MPYA

..

MATUKIO MBALIMBALI KUHUSU WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO BUNGENI MJINI DODOMA

Waziri wa Fedha na Mipango, mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akifafanua baadhi ya vipengele vya Muswada wa marekebisho ya Sheria mbalimbali Namba 4 ya Mwaka 2016, kuhusu marekebisho ya Sheria ya Mikopo, Misaada na Dhamana. Muswada huo ulipitishwa kuwa Sheria na Bunge Februari Mosi, 2017.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Bw. George Masaju, akihitimisha mjadala wa Muswada wa Marekebisho ya Sheria mbalimbali Namba 4 ya Mwaka 2016, uliopitishwa na wabunge kuwa Sheria Februari Mosi, 2017, Mjini Dodoma
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) na Naibu Waziri wake, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), wakipitia nyaraka za Muswada wa Marekebisho ya Sheria mbalimbali Namba 4 ya Mwaka 2016, Bungeni Mjini Dodoma, Muswada ambao tayari Bunge limeupitisha kwa kishindo kuwa Sheria Februari Mosi, Mjini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akimweleza jambo Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhe. Dkt. Medard Kalemani (Mb), nje ya viwanja vya Bunge mjini Dodoma, baada ya Bunge kupitisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria mbalimbali Namba 4 ya Mwaka 2016, Februari Mosi, 2017.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM).

Related Posts

Post a Comment