const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); Bodaboda 16 zang'olewa Matairi na Askari - HABARI MPYA

..

Bodaboda 16 zang'olewa Matairi na Askari


Agizo la Rais wa jamhuri ya muungano wa Dkt. John Pombe Magufuli la kulitaka jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani kung'oa matairi vyombo vyote vya moto vitakavyopita katika barabara za mabasi yaendayo haraka la tekelezwa kwa vitendo ambapo takribani pikipiki kumi na sita zimeng'olewa matairi na wahusika wakitarajiwa kufikishwa mahakamani hapo tarehe 2 febuari mwaka huu.

Agizo hilo la rais Magufuli alililoa kwa mara ya pili katika shughuli ya uzinduzi wa mradi wa mabasi yaendayo haraka lengo likiwa ni kuhakikisha miundombinu ya mradi huo haziharibiwi ambapo kamanda wa jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani nchini Mohamed Mpinga amesema zoezi hilo ni mwanzo tu na yeyote atakayetumia miundombinu hiyo hataonewa huruma.

Awadhi Haji ni mkuu wa kikosi cha usalama barabarani katika jiji la Dar es Salaam ambapo licha ya kukiri idadi kubwa ya waendesha bodaboda wamekuwa wakipita katika barabara hizo ameendelea kuwaasa watumiji wa vyombo vya moto kutambua miundombinu ya mradi huo ni kwa manufaa ya kila mtanzania hivyo kuna kila sababu ya kutunzwa na kila mtu.

Watuhumiwa wa makosa hayo na mengine ya uvunjifu wa sheria za barabarani pamoja na abiria wao wakiwa takribani sitini na moja baadhi ya waliozungumza na ITV licha ya kutokuwa na sababu za msingi za kutumia barabara hizo wamewahadharisha wenzao kwa kuwa adhabu iliyotajwa na Mh rais ni kweli inatekelezwa.

Watuhumiwa wote wakiwemo abiria wao wataendelea kukaa rumande hadi  febuari  2 mwaka huu watakapofikishwa mahakani.

Chanzo: ITV.

Wanging'ombe kujipanga kujenga soko la Nyanya tazama video hapo chini

Related Posts

Post a Comment