const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); ZIJUE NCHI 16 ZENYE HUDUMA BORA ZAIDI ZA AFYA DUNIANI - HABARI MPYA

..

ZIJUE NCHI 16 ZENYE HUDUMA BORA ZAIDI ZA AFYA DUNIANI


Taasisi ya utafiti ya Legatum ya nchini Uingereza imetoa jarida lenye matokeo ya utafiti unaohusu nchi zenye zaenye maendeleo zaidi duniani.

Taaisi hiyo imetumia vigezo 104 ili kupata nchi watakazo zifanyia utafiti. Moja ya vigezo vikubwa vya kuweza kuingizwa kwenye utafiti huu ni kuangalia afya ya watu wa nchi husika inaangaliwa kwa umakini kiasi gani.

Kwa mujibu wa taasisi hii, afya inapimwa kwa vigezo vitatu: afya ya msingi kuhusu mwili na akili, miundombinu ya kutoa huduma za afya pamoja na upatikanaji wa kinga mbalimbali dhidi ya magonjwa yanayoweza kupatiwa kinga.
Hizi ndio nchi 16 zinazoongoza kwa ubora wa huduma za afya:

16. Canada — Sheria ya afya ya mwaka 1984 inaitaka nchi hiyo kutoa bure huduma za afya na ziwe zinafikika kwa wananchi wote, mfumo huu unajulikana kama Medicare nchini humo. Hata hivyo kumekuwa na ongezeko la wananchi wa Canada kwenda Marekani kupata matibabu kwenye vituo binafsi vya afya kutokana na mfumo bado una dosari.


15. Qatar — Huduma bora zaidi kiafya katika nchi za Mashariki ya Kati zinapatikana nchini Qatar. Hivi karibuni nchi hiyo imechukua hatua kadhaa kuhakikisha huduma bora za afya zinapatikana kote nchini humo.


14. Ufaransa — Kwakuwa huwa inasifika sana kwa ubora wa huduma zake za afya, haishangazi kuiona nchi hii kuwa miongoni mwa vinara duniani. Kiwango cha kawaida cha mategemeo ya maishaya mtu nchini humo ni miaka 82.


13. Norway — Kiwango cha ubora nchini Norway kinakaribiana na kile cha Canada – majirani zao katika ukanda wa Scandinavia. Mara nyingi hukaribiana pia katika viwango vya ubora wa kidunia, moja ya sababu ikiwa ni afya bora za wananchi wake. Huduma za afya nchini humo hutolewa bure kwa watoto chini ya miaka 16, lakini watu wazima wanalipia. Serikali ya nchi hiyo inaongoza kwa kutumia fedha nyingi kwenye kuboresha afya za wananchi kuliko nchi yoyote ile duniani.


12. New Zealand — New Zealand ni moja ya nchi zenye wanamichezo wengi zaidi duniani, ikiwa na inatoa washiriki wengi sana katika mashindano ya michezo ya kimataifa. Kiwango cha chini cha maisha kwa mwananchi wa kawaida nchini humu ni miaka 81.6.


11. Ubelgiji — Umri wa kuishi kwa mwananchi wa kawaida ni miaka 81.1. huduma bora za afya zinapatikana nchi nzima , na pia sheria inawataka wananchi wote wawe bima ya afya.


10. Ujerumani — Japokuwa watu wa Taifa hili wanapenda sana bia na soseji, Wajerumani ni miongoni mwa watu wenye afya bora zaidi duniani. Kiwango cha maisha kwa mwananchi wa kawaida nchini humo ni miaka 81


9. Israeli — Israeli ni nchi inayoongoza katika nchi zote za ukanda wa Mashariki ya Kati kwa kutimiza vigezo vingi vilivyotumika katika utafiti huu. Nchi hiyo ipo nafasi ya nane katika nchi ambazo wananchi wake wa kawaida wanaishi kwa umri mkubwa zaidi duniani ambao ni miaka 82.5


8. Australia — Wakiwa na hali ya hewa nzuri sana na uwepo mdogo wa uharibifu wa mazingira, haishangazi kuona nchi hii kuongoza kwa ubora wa afya katika chi za ukanda ncha ya kusini mwaa dunia. Kiwango chake cha chini kwa maisha ya mwananchi wa kawaida ni miaka is 82.8, ambayo ni nafasi ya nne duniani kwa kigezo hicho.

7. Hong Kong — Mji mdogo sana wa Hong Kong una hospitali 11 za binafsi na 42 za serikali zinazowahudumia wananchi wake wapatao milioni 7.2. Mwaka 2012, wanawake nchini Hong Kong walikuwa na umri mkubwa zaidi wa maisha ikilinganishwa na sehemu yoyote ile duniani.


6. Swiden — Kama ilivyo kwa viwango vyote vya maisha na afya, nchi zilizopo Kaskazini nwa bara la Ulaya kama Swiden zinashika nafasi ya juu. Sweden inashika nafasi ya nne duniani kwa wanaume nchini humo kuwa na kiwango kikubwa zaidi cha uhai ikilinganishwa na nchi yoyote – wakiishi kwa wastani wa miaka 80.7


5. Uholanzi — Mwaka 2015 Uholanzi ilishika nafasi ya kwanza katika jarida moja linalochunguza ubora wa mifumo ya utoaji wa huduma za afya katika nchi za ulaya, ikipata alama 916 kati ya alama 1,000.

Wafanyakazi wakitafuta maua yaliyokufa katika mashamba ya maua yaliyopo jijini Noordwijk

4. Japani — Kiwango cha maisha kwa mwananchi wa kawaida ni miaka 83.7 — ambacho ndio kiwango kikubwa zaidi duniani.


3. Uswisi — Nchi tajiri, nzuri na yenye watu wenye afya bora sana. Uswisi ni nchi yenye kila kitu ambacho mtu angependa kiwepo nchini kwake. Huduma zake za afya zinapatikana nchi nzima na hupatikana kwa wananchi kulazimika kisheria kuwa na bima ya afya.

Wafanyakati wakiandaa uwanja wa michezo ya mieleka kabla ya kuanza kwa Tamasha la Taifa la mchezo wa Mieleka mwaka 2016.

2. Singapore — Hii ni nchi nyengine ambayo ni sawa na mji mdogo kuwepo katika nafasi za juu duniani. Ni nchi yenye watu milioni 5.6, ina kiwango cha chini cha maisha ya mwananchi wa kawaida ya miaka 83.1

Mji mkuu wa kibiashara nchini Singapore kama unavyoonekana nyakati za jioni

1. Luxembourg — Ni nchi ipo katikati ya nchi tatu za Ubelgiji, Ufaransa na Ujerumani na utajiri iliyonayo umechangia sana kuifanya iwe nafasi ya kwanza katika utafiti huu. Kiwango cha chini cha maisha ya mwananchi wa kawaida wa Luxembourg ni miaka 82.

Mji mkuu wa Luxembourg, Luxembourg City nyakati za baridi kali. Picha na Barbara Tasch

Related Posts

Post a Comment