Kiongozi wa muda mrefu wa Gambia, Yahya Jammeh amesema kuwa ataondoka madarakani ikiwa ni baada ya kung’ang’ania madarakani kufuatia kushindwa katika uchaguzi mkuu uliofanyika Disemba 1 mwaka jana.
Kupitia runinga ya Taifa, Yahya Jammeh amesema kuwa ataondoka kwani hakuna umuhimu wa hata tone la damu kumwagika.
Jammeh ameiongoza Gambia kwa muda wa miaka 22 lakini alishindwa katika uchaguzi wa Disemba 1 mwaka jana na kiongozi wa upinzani, Adama Barrow.
Adama Barrow akila kiapo kuwa Rais Gambia katika ubalozi wa nchi hiyo mjini Dakar nchini Senegal
Adama Barrow aliondoka nchini Gambia na kwenda Senegal ambapo ni nchini jirani na kuapishwa kuwa Rais wa Gambia katika ubalozi wa nchini hiyo mjini Dakar. Sherehe hiyo zilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kimataifa na wawakilishi kutoka umoja wa mataifa.
Majeshi ya nchini wananchama wa ECOWAS yalikuwa tayari katika mipaka ya Gambia tayari kumuondoa Yahya Jammeh kwa nguvu kufuatia kukataa kuondoka kwa hiari. Kiongozi wa Jeshi Gambia alisema hatowaamuru wanajeshi wake kuwazuia wanajeshi wa ECOWAS sababu mgogoro huo ni wa kisiasa na hawawezi kuingilia.
Uamuzi wa Jammeh umekuja muda mfupi baada ya mazungumzo na Marais wa Guinea na Mauritania.
Yahya Jammeh akitoka madarakani ataondoka nchini Gambia na haijelezwa atakwenda wapi.
Post a Comment
Post a Comment