const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); LADY JAYDEE AFUNGUKA JUU YA PENZI LA GADNER - HABARI MPYA

..

LADY JAYDEE AFUNGUKA JUU YA PENZI LA GADNER


aliamua kuachana na mahusiano yake ya zamani ambayo yalidumu kwa miaka mingi na kuamua kusonga mbele kwakuwa hayakuwa na faida kwake.

Mwanadada mkongwe wa muziki wa muziki wa Bongo Fleva, Lady Jaydee amedai wanawake wengi ni waoga wa kuanza maisha mapya ya mahusiano.

Jaydee ambaye kwa sasa ameingia kwenye mahusiano mapya ya kimapenzi na Spicy wa Naijeria baada ya kuachana na mumewe wa zamani, Gadner G. Habash aliyekuwa naye kwa takriban miaka 13.

Hata hivyo, mwanadada huyo amefunguka kuwa watu wengi wanapokuwa kwenye mahusiano kuna maisha wanakuwa wameyatengeneza, hivyo inakuwa ngumu kuondoka na kuyaacha.

Wanawake wengi wanashindwa kutoka kwenye mahusiano, kwenye ndoa zisizo na afya kutokana na wao kutojiamini. “Kwanza si jambo rahisi sana kama umekaa na mtu muda mrefu halafu uamue tu kuwa unaondoka.” alisema.

Ameongeza kuwa kwa upande wake aliamua kuachana na mahusiano yake ya zamani ambayo yalidumu kwa miaka mingi na kuamua kusonga mbele kwakuwa hayakuwa na faida kwake.

HT – Majira

Related Posts

Post a Comment