const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); Wazee maarufu Mtwara Waikumbusha Serikali ahadi zake za wakati wa gesi - HABARI MPYA

..

Wazee maarufu Mtwara Waikumbusha Serikali ahadi zake za wakati wa gesi


Wazee maarufu wa mkoa wa Mtwara wamemaliza mwaka kwa kuikumbusha serikali kutekeleza ahadi zake za kuuletea mkoa wa Mtwara maendeleo kutokana na uwepo wa rasilimali ya gesi asilia walizoahidiwa wakati serikali inafanya mchakato wa kusafirisha gesi kutoka mkoani humo kwenda Dar e Salaam.
Wazee hao wamewasilisha maombi hayo kwa mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi CCM mkoani humo Mohamed Sinani ili aweze kuyawasilisha kwa viongozi wa serikali kuu ambayo iliahidi kuwaletea maendeleo wakazi wa Mtwara.
wazee maarufu wakiwa na baadhi ya vijana wakiongozwa na aliyewahi kuwa mbunge wa Jimbo la Mtwara Mjini,ambae sasa ni diwani kata ya Libobe Alhaji Mzee Rashidi Mpeme wanasema kuwa mwaka wa 2016 umeisha salama pasipokuwa na vurugu ndani ya mkoa wao.Kwa kutambua amani iliyopo nchini wazee hao wanatoa salamu za pongezi kwa Rais Dk. John Pombe maghufuli kwa kuonesha dhamira ya dhati ya kuwaletea watanzania maendeleo.

Licha ya pongezi hizo wazee wanasema katika suala la maendeleo mkoa wa Mtwara umesahaulika na ahadi zilizoahidiwa wakati wa Gesi zimesahaulika pia

Related Posts

Post a Comment