MAELFU ya wapambe wa bwana harusi waliokuwa wanajiandaa kusherekea harusi ya ndugu yao wamejikuta wakipigwa na kumbuwazi baada ya kupata taarifa kwamba biharusdi mtarajiwa ameingia mitini saa chache kabla ya kufanyika harusi .
Biharusi huyo mkaazi wa Kivumoni Msuka Wilaya ya Micheweni hadi sasa hajulikani alipo baada ya kutoweka nyumbani usiku wa manane wa siku ya kuamkia Jumatano ya januari 11 siku ambayo ilikuwa ifanyike harusi .
Akizungumza kwa masikitiko bwana harusi Ali Helef amesema kitendo cha biharusi kutoroka kimemsababishia hasara kubwa kwani alikuwa amefanya maandalizi ikiwa ni pamoja na kuwapokea jamaa zake kutoka Dodoma , Dar es Salaam na Unguja .
Amesema pamoja na biharusi kutoweka , lakini amewaomba wanafamilia ya binti huyo kumtafuta ili amuowe kwani hasara aliyopata ni kubwa .
“Mimi nataka kuowa na vyema biharusi atafutwe ili niowe kwani nimeingia gharama sana kufanya maandilizi ikiwa ni pamoja na kuwapokea jamaa zangu kutoka Unguja na Bara ”alisema .
Aidha kwa upande wa Familia ya Bwana Harusi wamesema bado hawajakaa kama familia ili kutafuta ufumbuzi wa suala hilo na kwamba wanatarajia kukutana mwishoni wa wiki ili kutoa maamuzi juu ya suala hilo.
Akizunzgumza na mwandishi wa habari hizi msemaji wa familia hiyo Abdalla Ali amesema suala hilo wamepanga kulimaliza pindi wakatapo kutana pande zote mbili akiamini kwamba ndani ya familia na biharusi sio wote wanaounga mkono kitendo hicho .
“Sisi kama familia bado hatujakaa kulijadili na tunatarajia kukutana na upande wa biharusi kwani tunaamini ndani ya familia hiyo siyo wote walikifurahia kitendo hichi , tutoa maamuzi yetu baada ya kukutana ”alifahamisha .
Kwa upande wa biharusi mwandishi wa habari hizi hakupata mashirikiano baada ya kuambiwa baba mwenye nyumba kaondoka na hajulikani aaliko na muda atakaorudi .
Hata hivyo majirani wameelezea kusikitishwa na kitendo hicho na kusema iwapo upande wa biharusi walikuwa hawakubaliani ni bora wangetoa taarifa mapema kabla ya bwanaharusi kufanya maandalizi .
Aidha taarifa ambazo zimepatikana na mmoja wa wanafamilia ya bwanaharusi zinasema iwapo watashindwa kukubaliana na upande wa biharusi watafungua kesi ya
Post a Comment
Post a Comment