Taarifa zilizotufikia hivi punde zimeeleza kuwa, chanzo cha moto mkubwa uliozuka usiku wa kuamkia leo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar es Salam na kusababisha shughuli zote za usafirishaji Uwanjani hapo kusimama kwa muda, kimejulikana kuwa ni hitilafu ya umeme.
Akizungumza na mtandao wa Global Publshers mapema asubuhi ya leo, Kamanda wa Polisi wa Viwanja vya Ndege, ACP Martin Otieno amesema kuwa, uchunguzi umebaini kwamba, kulikuwa na tatizo la umeme ambalo hata hivyo lilishughulikiwa mara moja.
“Kulikuwa na tatizo la umeme kwenye eneo la kuhifadhia mizigo lakini moto ulidhibitiwa vizuri na sasa shughuli zinaendelea kama kawaida japokuwa bado tunatumia Terminal One (uwanja wa zamani) kwa kuwabeba abiria kwenye mabasi na kuwapeleka panapohusika.
“Kwa sasa ndege zote zinatua na kuruka bila tatizo lolote na kufuatana na ratiba hivyo hakuna hofu yoyote kwani muda si mrefu eneo hilo la mizigo litakuwa limeshawekwa sana, ” alisema Kamanda Otieno.
Aidha Mamlaka ya Uwanja huo imetoa mabasi kwa ajili ya kubeba abiria kuwapeleka Terminal One ambako shughuli za usafirishaji zinaendelea kama kawaida.
Post a Comment
Post a Comment