const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); MAJALIWA AHUTUBIA MKUTANO WA HADHARA MJINI NJOMBE PIA ATEMBELEA MAJENGO YA POLISI YANAYOJENGWA LUDEWA - HABARI MPYA

..

MAJALIWA AHUTUBIA MKUTANO WA HADHARA MJINI NJOMBE PIA ATEMBELEA MAJENGO YA POLISI YANAYOJENGWA LUDEWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka kesho awapeleke wakaguzi wa heshabu kwenda kukagua mapato na matumizi ya Mamlaka ya Maji ya Mji wa Njombe (NJUWASA).

Ametoa agizo hilo leo (Ijumaa, Januari 27, 2017) wakati akizungumza na wananchi katika mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya Sekondari Mpechi, Halmashauri ya Mji wa Njombe.

Waziri Mkuu amesema wakaguzi hao mbali na kukagua mapato na matumizi ya mamlaka hiyo pia waangalie kama wananchi walihusishwa katika ukokotoaji wa gharama za malipo ya bili za maji.

Ametoa agizo hilo baada ya wananchi kuilalamikia mamlaka hiyo kupitia mabango kwamba wanatozwa bili kubwa ya maji licha ya huduma hiyo kupatikana kwa kusuasua katika mji huo.

Kufuatia malalamiko hayo Waziri Mkuu alimtaka Mkurugenzi Mtendaji wa NJUWASA, Bw. Daudi Majani kutoa ufafanuzi juu ya jambo hilo ambapo alisema kwa mwezi wanakusanya sh. milioni 75 zinazotumika kuendeshea na uboreshaji wa huduma.

“Maji hakuna unasema unaboresha unaboresha huduma gani? Wananchi wanalalamika maji hakuna na mnawatoza gharama kubwa, Mkuu wa Mkoa kesho peleka wakaguzi wakakague kwa mwezi anakusanya kiasi gani na anafanyia nini,”

Wakati huo huo, Waziri Mkuu amewataka watumishi wa umma kujiwekea utaratibu wa kwenda kwa wananchi na kusikiliza changamoto mbalimbali zinazowakabili ili kuzitafutia ufumbuzi badala ya kujifungia maofisini.

“Uwepo wa mabango mengi kwenye mikutano ya hadhara ya viongozi ni ishara tosha kwamba watendaji hamuendi kwa wananchi kuwasikiliza kero zao. Mabango mengi hapa si ya Waziri Mkuu ni hapahapa,” amesema.17.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa mpira wa shule ya sekondari ya Mpechi mjini Njombe Januari 27, 2017.
Mmoja wa wananchi waliofika kwenye uwanja wa mpira wa Shule ya Sekondari ya Mpechi mjini Njombe akitoa dukuduku lake kwa njia ya karatasi wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipohutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa mpira wa Shule ya Sekondari ya Mpechi, Januari 27, 2017. 
Wananchi wa Mji wa Njombe wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa mpira wa Shule ya Sekondari ya Mpechi Januari 27, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wa mji wa Njombe wakati alipowasili kwenye uwanja wa mpira wa Shule ya Sekondari ya Mpechi kuhutubia mkutano wa hadhara Januari 27, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua nyumba za Askari Polisi ambazo kwa muda mrefu hazijakamilika katika mji wa Ludewa Januari 27, 2017.

Related Posts

Post a Comment