Makau Kioko (53) anamiliki shamba analofuga nyoka hatari aina ya Cobra ambapo makosa kidogo tu katika kuwashika nyoka hawa yanaweza yakagharimu maisha yake. Ingawa anavaa glovu mikononi wakati wa shughuli zake hizi,nyoka aina hii akimng’ata sehemu nyengine yoyote inaweza kumsababishia kifo ndani ya dakika 15 tu.
Sumu hiyo kali inayotengenezwa na aina hii ya nyoka husababisha mtu aliyeng’atwa kushindwa kupumua, mwili kupooza na mwisho kufariki sunia. Sumu inayotolewa na nyoka hawa ni kali kiasi cha kuwa na uwezo wa kumuua tembo.
Bwana kioko ni mmiliki wa shamba hili la nyoka na kituo cha maonyesho kinachojulikana kwa jina la Kioko Snake Ventures, kilichopo Kitui, mashariki mwa Kenya.
Mmoja wa wafanyakazi wake alifariki kutokana na majeraha baada ya kuvunjwa na nyoka aina ya chatu, nyoka mwenye umbo kubwa zaidi barani Afrika.
“Chatu alihisi anatishiwa uhai wake wakati mfanyakazi alipokuwa anajaribu kupeleka mbuzi aliye hai kama cchakula cha nyoka huyu,” alisema Kioko.
“Kwa haraka sana chatu alijiviringisha mwilini mwa mfanyakazi huyuna kumvunja. hakumla, ni mara chache sana utasikia chatu amekula binadamu, ila alifariki.”
Hadi sasa kuna mashamba na vituo vya aina hiyo 42 nchini Kenya, na vyengine 21 vinasubiri usajili, hii ni kwa mujibu wa mamlaka ya serikali inayohusika na usimamizi wa sekta hiyo (The Kenya Wildlife Service). Mashamba ya aina hii hutengeneza pesa kimsingi kutokana na viingilio vinavyolipwa na watalii.
Bwana Makau Kioko akiwa amebeba chatu kwa ajili ya kupiga picha
Pia husafirisha nyoka hawa kwenda nchi za Ulaya na Amerika Kaskazini, ambapo nyoka wakubwa na wakali zaidi huuzwa kwa zaidi ya shilingi za Kenya 10,000 ambazo ni zaidi ya dola za Kimarekani ($100). Pia nyoka hawa huuzwa kwa ajili ya kuvuna sumu wanazotengeneza na pia kutumika katika tafiti za kisayansi, nchini na nje ya nchi.
Makau Kioko (kushoto) na mmoja wa wafanyakazi wake wakiwa wameshika nyoka aina ya chatu
Kioko kwa sasa ana wafanyakazi 16 ambao kwa pamoja wana kazi ya kufuga zaidi ya nyoka 1,800, ambao nusu yao ni chatu. Nusu waliobaki wanajumuisha zaidi ya aina 32 za nyoka wanaopatikana barani Afrika, na aina nyengine 13 ambao wanapatikana kwenye mabara mengine.
Post a Comment
Post a Comment