Akiwa ziarani mkoani Simiyu ambapo alikwenda kufungua barabara miongoni mwa mambo mengi aliyoyazungumzia ilikuwa ni changamoto ya upatikana wa maji mkoani humo.
Rais Dkt Magufuli alitoa maagizo kwa Waziri wa Ardhi na Waziri wa Nishati kwa kushirikiana na uongozi wa Mkoa wa Simiyu kufuta leseni ya mwekezaji wa madini kama atakataa kutoa eneo yalipo madini hayo ili pawekwe tenki la maji litakalosaidia wakazi wa mkoa huo kupata maji.
Siku chache baada ya agizo hilo, uongozi wa mkoa huo ulikutana na kufanya mazungumzo na kampuni ya Dutwa Minerals Limited kuhusu ujenzi wa tenki hilo.
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu ikiwa katika mahojiano na wawekezaji wa mradi wa uchimbaji wa Nickle wa Dutwa. Wawekezaji hao, Dutwa Minerals Limited, wanatakiwa kutoa nafasi kuruhusu ujenzi wa tenki la maji, mradi utakaohudumia wakazi wa wilaya tatu za Mkoa huo. Mahojiano hayo yaliongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, RC Anthony Mtaka, Katibu Tawala Jumanne Sagini na kuwajumuisha wajumbe wote walioko ziarani jijini Dar es Salaam.
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu ikiwa katika mahojiano na wawekezaji wa mradi wa uchimbaji wa Nickle wa Dutwa.
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu ikiwa katika mahojiano na wawekezaji wa mradi wa uchimbaji wa Nickle wa Dutwa.
Post a Comment
Post a Comment