LEBO ya Wasafi Classic Baby (WCB) licha ya kukusanya vichwa vya wasanii wakali lakini nyota ya Richard Martin ‘Rich Mavoko’, imeendelea kung’ara ambapo kwa sasa anamake ‘headline’ kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari kutokana na ngoma yake ya Kokoro aliyomshirikisha bosi wake, Diamond Platinumz.
Ingawa ni miezi kadhaa tu tangu kuachiwa kwa Koko¬ro, imekuwa ikisumbua kwenye orodha za nyimbo ambazo zinafanya vizuri kwa kipindi hiki ikiwemo Muziki ya Darassa.
Kilinge imemtembelea nyota huyo katika Ofisi za WCB zilizopo Sinza- Mapambano ambapo hapa anafunguka mambo mengi zaidi:
KOKORO ILIKUWA INACHUNGUZWA NA BASATA KWA KUKOSA MAADILI, ULISHAAMBIWA?
“Hatujawahi kusikia suala la video yetu ya Kokoro kuchunguzwa na Basata (Baraza la Sanaa Taifa) na wala hatukupewa taarifa yoyote ile.
“Wanachotakiwa kukitambua Basata kwanza muziki kwetu sisi vijana ndiyo ajira ambayo inatufanya kuwa mbali na kuiba au kukaba mitaani na bila kuufanya huu sasa hivi tungekuwa majambazi.
“Pia wasiwe polisi kwa kufungia nyimbo zetu bali wawe wazazi au walezi na washauri lakini wanatakiwa watambue kwamba unapofungia wimbo wangu nimetumia kiasi gani kwenye ‘kushoot’, sasa watanirudishia vipi gharama zangu?
“Wao wanatakiwa kutuita na kutuambia hapa umekosea nini inabidi urekebishe kwa ajili ya wimbo husika kuendelea kupigwa na wasisahau tuna menejimenti ambazo zinatusimamia, hivyo wanatakiwa wawafuate na kuwaambia msanii wako amekosea na ajirekebishe, siyo kuchukua maamuzi tu ya kufungia video zetu.”
VIDEO YENU YA KOKORO KUNA VIPANDE VINAFANANA NA NGOMA YA LOVE ME YA LIL WAYNE, LIPOJE HILO?
“Sisi hatujamuiga mtu yeyote yule kwenye kutengeneza Video ya Kokoro na wala hatujui kama tumeiga wimbo wa Wayne kwa sababu sisi tulifanya ubunifu wetu na video kutoka kama inavyoonekana na kama imefanana basi mawazo yamegongana.”
Video ya Kokoro inafanana na ya Lil Wayne kwenye vipande vya Diamond akiwa ndani ya chumba chini kuna maji na akiwa amezungukwa na wadada wawili, sawa na Love Me ya Wayne pamoja na wadada wakiwa wanapaka damu kwenye ukuta, tofauti ni rangi ya maeneo pekee.
MAPOKEO YA KOKORO KWA JAMII, UNAJISIKIAJE?
“Kwenye ngoma ya Kokoro watu waelewe kwamba hakupangwa kufanya Diamond, kwa sababu alipangwa mtu mwingine tofauti na yeye lakini mwisho nikaona kwa nini nisumbuke wakati Diamond yupo na mimi nampata kiurahisi zaidi?
“Nawashukur u mashabiki kwani wameonyesha ku¬uelewa wimbo wenyewe mapema na kila unapopita basi wao wanauimba na kiukweli najisikia furaha kwa jinsi walivyouelewa kwani hayo ni mapokeo makubwa.”
WEWE UPO TIMU DIAMOND, UNAWEZA KUFANYA NA KIBA WIMBO WOWOTE?
“Kwa nini nisifanye naye kama nitaona kuna biashara na mimi nitapata kitu fulani kutoka kwake?
Nipo tayari kabisa kufanya naye na wala hakuna tatizo lolote.”
MALENGO YAKO NI KUENDELEA KUBAKI WCB?
“Kwa sasa siwazi kuondoka hapa WCB lakini kwa baadaye itakavyokuja kutokea naweza kuondoka kama watajitokeza watu watakaoweza kuvunja mkataba wangu na kama viongozi wa hapa wakiridhia, basi hakuna linaloshindikana.”
WASANII GANI WA NJE YA TANZANIA UNAFIKIRIA KUFANYA NAO KOLABO?
“Wapo wengi lakini Wizkid natamani sana kufanya naye kolabo kwa sababu nilianza kumfuatilia tangu kitambo sana, tangu enzi za Halla It Boy lakini pia Davido ambapo naamini nikifanya nao, muziki wangu utakua kutoka ul-ipo hapa.”
TOFAUTI GANI ILIYOPO KATI YA KUWA PEKE YAKO NA KUMILIKIWA NA LEBO?
“Kwanza watu waelewe nimekuja hapa kwa ajili ya bi¬ashara na hiyo ndiyo inaendelea kuniweka hapa, lakini pia uto¬fauti upo kwa sababu zamani kila kitu nilikuwa nafanya mimi kuanzia kurekodi hadi kushuti video lakini kwa sasa kila kitu kinafanywa na uongozi ambapo kazi yangu kubwa ni kuandaa ‘idea’ ya wimbo na baada ya hapo kila kitu kinafanywa na wao ambao watahangaika na mambo yote.
“Lakini hapa kuna mchanganyiko wa wasanii wengi Harmonize, Rayvany, Q Boy na wengineo ambao wamekuwa msaada kwangu pale ninapoandika wimbo au kutaka kufanya jambo lolote. Huwa wananipa ushauri na kuniongezea baadhi ya vitu juu ya kuvifanya na kuboresha.”
VIPI KUHUSU FAMILIA, UNA MKE AU MTOTO?
“Mambo yangu ya kimahusiano huwa sipendi kuyaweka hadharani sana ila muda wake ukifika kila mtu atamjua nani natoka naye lakini nina mtoto mmoja anayeitwa Wenslaus ‘Wency’.”
Chanzo:GPL
Post a Comment
Post a Comment