Nchi jirani zimetishia kupeleka vikosi vya majeshi yao nchini Gambia baada ya Rais wa nchi hiyo, Yahya Jammeh kukataa kutoka madarakani baada ya muda wake wa uongozi kuisha. Mpinzani wake, Bwana Adama Barrow, aliyeshinda katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo uliofanyika mwezi uliopita anatakiwa kuapishwa kushika nafasi hiyo ya urais.
Majeshi ya nchi za magharibi mwa Afrika yapo tayari kutoa msaada wa kijeshi kumuondoa madarakani Jammeh. Rais wa Mauritania, Mohamed Ould Abdel Aziz hakuweza kufikia suluhu baada ya kufanya mazungumzo na Rais huyo aliyemaliza muda wake.
Rais Aziz alikwenda jijini Banjul Jumatano na kukutana kwa mazungumzo na Rais Jammeh kabla ya kwenda jijini Dakar kwa mazungumzo zaidi na Rais mteule wa Gambia, Adama Barrow na Rais wa Senegal, Macky Sall.
Majeshi ya Senegal bado yapo katika mpaka wa nchi yake na Gambian japokuwa muda wa Rais Jammeh kuwepo madarakani umeshakwisha tokea jana usiku. Naijeria pamoja na nchi nyengine za ukanda huo zinaunga mkono uamuzi wa kutoa msaada wa kijeshi nchini Gambia.
Pamoja na tishio hilo la kijeshi, Mkuu wa Majeshi nchini Gambia, Ousman Badjie amesema vikosi vyake havitapigana hata kama vikosi vya Senagal vikiingia ndani ya mipaka ya Gambia, aliliambia shirika la habari la AFP.
“Hatutajihusisha na mapambano ya kijeshi kwakuwa huu ni mgogoro wa kisiasa,” he said. “sitaki askari wangu wahusike kwenye mapigano ya kipuuzi. Nawapenda vijana wangu.”
Rais Jammeh ametawala nchi hiyo tangu mwaka 1994 alipoichukua kutokana na mapinduzi ya kijeshi.
Rais wa Gambia aliyemaliza muda wake,Yahya Jammeh
Rais Mteule wa nchi hiyo, Bwana Adama Barrow anatarajiwa kuapishwa kushika nafasi hiyo akiwa nchini Senegal. Shughuli hiyo itafanyika katika Ubalozi wa Gambia jijini Dakar, Senegal jioni hii.
Rais mteule wa Gambia anayetarajiwa kuapishwa nchini Senegal, Adama Barrow.
Post a Comment
Post a Comment