const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); KOREA KASKAZINI YAONGEZA SHUGHULI ZA KUTENGENEZA NYUKLIA - HABARI MPYA

..

KOREA KASKAZINI YAONGEZA SHUGHULI ZA KUTENGENEZA NYUKLIA


Picha za satelaiti zimeonesha kuongezeka kwa shughuli katika kinu kikuu cha kuzalisha nyuklia nchini Korea Kaskazini.

Kituo cha Marekani kinachofatilia matukio katika eneo hilo kimesema kuna uwezekano wa serikali ya Korea Kaskazini inataka kuanza upya uzalishaji wa silaha katika kituo cha Utafiti wa Kisayansi cha Nyuklia (Yongbyon Nuclear Scientific Research Center) kilichopo umbali wa kilomita 90 kutoka mji mkuu Pyongyang.

“Shughuli katika kituo hiki sasa zimeongezeka kwa zaidi ya mara tano ya kiwango chake cha kawaida kilichokuwa kimezoeleka kwa miaka matano iliyopita,” imesema ripoti hiyo.

“Matokeo kutokana ongezeko la vitendo hivyo bado hayajafahamika bali hilo linathibitisha kuwa kinu cha Yongbyon kinabaki kuwa kitovu cha kuendesha program za nyuklia nchini Korea Kaskazini.”

Rais Kim Jong-un wa Korea Kaskazini akipungia mkono vikosi vya majeshi ya nchi yake

Related Posts

Post a Comment