const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); Prof Muhongo afunguka juu ya tuhuma za kuhusika na kushiriki kikao cha kupandisha bei yaUmeme..!! - HABARI MPYA

..

Prof Muhongo afunguka juu ya tuhuma za kuhusika na kushiriki kikao cha kupandisha bei yaUmeme..!!

WIZARA ya Nishati na Madini imekanusha taarifa kwamba Waziri wake Profesa Sospeter Muhongo katika kikao chake na Benki ya Dunia (WB) kilichofanyika Septemba 28 mwaka jana kilijadilii mchakato wa kupandisha bei ya umeme nchini.

Imeeleza katika taarifa yake kwamba katika kikao hicho walijadili masuala ya upatikanaji wa umeme wa kutosha, uhakika na bei nafuu kwa ajili ya kuchochea shughuli za maendeleo ya kukuza uchumi wa nchi , kuongeza ufanisi wa utendaji wa Shirika la Umeme (TANESCO) na kupunguza deni la TANESCO.

Aidha katika taarifa kwa umma iliyotolewa jana na Wizara hiyo ilieleza kuwa taarifa iliyotolewa na gazeti moja la kila siku kwa siku mbili mfululizo kuwa Waziri Muhongo alishiriki katika kikao na ujumbe wa Benki ya Dunia kilichofanyika siku hiyo kilichojadili kupandishwa kwa bei ya umeme, si ya kweli.

Wizara ilieleza kuwa wamekuwa wakifanya vikao na wadau mbalimbali zikiwemo Taasisi za Umma, Binafsi na Washirika wa Maendeleo yakiwemo Mashirika ya Kifedha ya Kimataifa kwa lengo la kuhamasisha uwekezaji katika Sekta za Nishati na Madini nchini.

Taarifa hiyo ilifafanua kwamba siku hiyo ya Septemba 28 mwaka jana kulifanyika kikao na ujumbe kutoka Benki ya Dunia ikiwa ni mwendelezo wa vikao vya majadiliano kuhusu upatikanaji wa mkopo wa Dola za Marekani milioni 200 kwa ajili ya kuboresha uendeshaji wa Shirika la Ugavi wa Umeme (TANESCO).

Taarifa hiyo ilieleza kuwa kikao hicho pia kilihudhuriwa na taasisi nyingine zikiwemo Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Shirika la Maendeleo la Petroli Tanzania (TPDC), Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA).

Katika kikao hicho walijadili masuala ya upatikanaji wa umeme wa kutosha, uhakika na bei nafuu kwa ajili ya kuchochea shughuli za maendeleo ya kukuza uchumi wa nchi ikiwemo viwanda, biashara, kilimo na huduma za jamii, kuongeza ufanisi wa utendaji wa Shirika la Umeme (TANESCO) na Kupunguza deni la TANESCO.

Taarifa hiyo ya wizara ilieleza kuwa katika kulipunguza deni la TANESCO ambalo linakaribia Sh bilioni 800 (takriban Dola za Marekani milioni 363) na kuboresha shughuli za utendaji za TANESCO, Benki ya Dunia ilijadiliana na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara hiyo ili kupata mkopo wa Dola za Marekani milioni 200.

“Hivyo, katika kikao hicho, hakukuwa na makubaliano ya kupandisha bei ya Umeme kama ilivyoripotiwa na gazeti hilo,Vile vile, tunaomba kuutaarifu Umma kwamba Wizara ya Nishati na Madini kwa niaba ya Serikali inafanya majadiliano na Benki ya Maendeleo ya Africa (AfDB), Umoja wa Ulaya (EU), JICA (Japan), na Mashirika mengine ya fedha kwa lengo la kutafuta fedha za kuboresha Sekta ya Nishati,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Related Posts

Post a Comment