const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); Picha/Video: Wacheza dansi 50 wafunga mtaa kwa kutumbuiza juu ya magari kusherehesha mazishi ya mwanasiasa - HABARI MPYA

..

Picha/Video: Wacheza dansi 50 wafunga mtaa kwa kutumbuiza juu ya magari kusherehesha mazishi ya mwanasiasa

Wacheza dansi wa kike kwenye kumbi za usiku wapatao 50, wakiwa wamevalia vivazi vyeusi wamewaacha na mshangao wapita njia wakati wakiusindikiza mwili wa mwanasiasa mmoja aliyefariki mwezi Decemba nchini Taiwan.

Kwenye msafara wanawake hao wakiwa juu ya magari ya aina ya “Jeep”, yenye rangi tofauti walikuwa wakicheza na kuimba na kusababisha foleni kubwa ya magari barabarani na watu wengi kubaki wakiwashangaa, kwa kuwa ni kinyume na tamaduni za huko.

Waendesha pikipiki nao waliufuatilia msafara wakiwashangaa wanawake hao. Familia ya mwanasiasa huyo imesema, marehemu Tung Hsiang aliagiza kufanyika namna hiyo, kwa kuwa alipendelea mambo kama hayo.





Related Posts

Post a Comment