Barua zilizoandikwa kwa mkono na marehemu Princess Diana zimeuzwa kwa maelfu ya pound kwenye mnada uliofanyika Alhamis hii nchini Uingereza.
Barua hizo sita zilitumwa kwa Cyril Dickman, aliyekuwa mwangalizi mkuu wa ikulu ya Buckingham miaka ya 1980 na 1990. Katika barua moja iliyotumwa siku tano baada ya kuzaliwa kwa Harry, September 1984, Diana alimshukuru Dickman kwa kadi aliyomtumia na kueleza jinsi Prince William alivyokuwa akimpenda mdogo wake.
“William adores his little brother and spends the entire time swamping Harry with an endless supply of hugs and kisses, hardly letting the parents near!” aliandika.
Barua hiyo iliuzwa kwa paundi 3,200. Diana alifariki kwa ajali ya gari mjini Paris mwaka 1997.
Post a Comment
Post a Comment