Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 28 Januari, 2017 aliondoka nchini na kuelekea Mjini Addis Ababa nchini Ethiopia ambako anahudhuria mkutano kilele wa 28 wa wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Umoja wa Afrika (AU) unaoendelea nchini humo.
Pamoja na kuhudhuria Mkutano huo, akiwa Addis Ababa Rais Magufuli anatarajiwa kukutana na kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali wa Bara la Afrika wanaohudhuria Mkutano huo.
Hapa chini ni picha mbili za Rais Dkt Magufuli akiwa katika vikao nchini Ethiopia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Manuel Olveira Guterres wakati alipokuwa kwenye mojawapo ya vikao vya Umoja wa Afrika (AU) vinavyofanyika katika Makao makuu yake mjini Addis Ababa nchini Ethipia. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Augustine Mahiga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakati alipokuwa kwenye mojawapo ya vikao vya Umoja wa Afrika (AU) vinavyofanyika katika Makao makuu yake mjini Addis Ababa nchini Ethipia. PICHA NA IKULU
Post a Comment
Post a Comment