const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); PICHA 10: NAMNA WAZIRI JANUARY MAKAMBA ALIVYOADHIMISHA SIKU YAKE YA KUZALIWA - HABARI MPYA

..

PICHA 10: NAMNA WAZIRI JANUARY MAKAMBA ALIVYOADHIMISHA SIKU YAKE YA KUZALIWA


Januari 28 kila mwaka ni kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, na Mbunge wa Bumbuli, January Yusuf Makamba.

Katika siku yake ya kuzaliwa mwaka 2017, Waziri Makamba aliiadhimisha kiutofauti ambapo alikwenda jimbo kwake na kushiriki shughuli mbalimbali na wapiga kura wake.

Waziri Makamba alipata nafasi ya kushiriki shunguli za ujenzi jimboni Bumbuli lakini pia alifanya vikao na watu mbalimbali vyenye lengo la kujadili mustakabali wa maendeleo ua jimbo hilo.

Mbali na hayo Waziri Makamba alitembelea baadhi ya shule za msingi jimboni humo na kuzungumza na wanafunzi huku akiwahimiza kuweka bidii kwenye masomo yao kwani Bumbuli na Tanzania inawategemea wao kuja kuwa wataalamu wa baadae wakuisaidia.

Katika kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa kwa mwaka 2017, Waziri January Makamba anatimiza umri wa miaka 43. Alizaliwa tarehe 28 Januari 1974 mkoani Singida.

Hapa chini ni picha za matukio mbalimbali ya Waziri Makamba alivyoadhimisha siku yake ya kuzaliwa.

C

Related Posts

Post a Comment