Shirika la Kijasusi Nchini Marekani (CIA) limechapisha mtandaoni zaidi ya kurasa milioni 12 za nyaraka ambazo baadhi yake zinaonyesha kuwa mashushushu wa shirika hilo waliwahi kuichunguza Tanzania.
Nyaraka hizo zilizochapishwa juma lililopita zinaonyesha nyaraka za siri za kipindi cha nyuma za shirika hilo kuhusu ushawishi wa China katika masuala ya kijeshi, kisiasa na kiuchumi nchini Tanzania na utendaji kazi wa Rais wa Kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Nyaraka hizo zinaonyesha namna CIA walivyokuwa wakimtazama Nyerere kwa utofauti na dunia ilivyokua ikimtazama kama kiongozi imara mwenye heshima duniani na kuongozi wa harakati za ‘Pan Africanism.’
Aidha, nyaraka hizo zinaonyesha kuwa suala la Marekani kushindwa kuwa na ushawishi juu ya Nyerere lilikuwa jambo lililowasumbua sana enzi za utawala wake licha ya kuwa Nyerere alikuwa mmoja wa wahitimu wa elimu ya magharibi.
Kipindi cha sera za Ujamaa na Kujitegemea, Marekani ilionekana kutokufurahia uhusiano mzuri uliokuwapo kati ya Tanzania na China kwani waliona kuwa China wanayo nafasi kubwa ya ushawishi kuliko wao.
Wakati sera za ujamaa zikikumbwa na changamoto mwaka 1985 na Rais Mwl. Nyerere akifikia mwisho wa uongozi wake, CIA walieleza kuwa huenda Mwl. Nyerere asiondoke madarakani licha ya kuwa aliwahi kutangaza kuwa angeondoka sababu kubwa ikiwa hajui ni nani atakayerithi kiti hicho kufuatia kifo cha Waziri Mkuu Sokoine aliyefariki Aprili 12, 1984 kwa ajali ya gari aliyedaiwa kuwa atakuwa Rais wa pili wa Tanzania.
Lakini sababu nyingine iliyoelezwa na CIA ya Nyerere kuweza kubaki madarakani ni sababu sera za ujamaa kwa wakati ule kuwa zilikuwa zikikabiliwa na changamoto kubwa ya utandawazi na soko huria.
Hapa chini ni nyaraka ya CIA wakimuelezea Mwl. Julius Nyerere na uongozi wake.
Nyaraka nyingine zilizotolewa na CIA
Kuweza kuona nyaraka zaidi bonyeza
Post a Comment
Post a Comment